Monday, 16 February 2015

Misri kulipiza kisasi mauaji dhidi ya Wakristo

Misri kulipiza kisasi mauaji dhidi ya Wakristo

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri
Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri
Rais wa Misri amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kwa namna yoyote ile inayoona inafaa katika kulipiza kisasi cha mauaji ya kundi la Wakristo wa madhehebu ya Coptic yaliyofanywa na kikundi cha wapiganaji wa jihad nchini Libya wenye uhusiano na kikundi cha Islamic State.
Rais Abdel Fattah al-Sisi ametoa kauli yake kupitia televisheni ya taifa baada ya video moja kuonyesha mateka wapatao kumi wa kundi la waumini wa madhehebu ya Coptic kukatwa vichwa.
Waumini ishirini na mmoja wa madhehebu ya Coptic nchini Misri walitekwa nchini Libya wiki kadhaa zilizopita. Maandishi yaliyowekwa katika video hiyo yanaonyesha walilengwa kwa sababu ya dini yao. Misri imetangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu hao.
Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,  Al Azhar   imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya “kinyama”. Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.

clouds stream