Obasanjo atimuliwa PDP, achana kadi yake hadharani kwa hasira
Mgogoro umeibuka ndani ya chama tawala cha PDP kufuatia Rais wa
Zamani Bw. Olusegun Obasanjo kutimuliwa ndani ya chama kwa madai ya
kupinga vikali kuahirishwa kwa uchaguzi nchini Nigeria hadi mwezi machi.
Muda mchache kabla ya kutimuliwa chamani, Obasanjo aliwaambia waandishi wa Habari kuwa alikuwa akitarajia kutimuliwa chamani japo ujumbe ulimfikia mapema kabla ya tangazo.
Kwa hasira alichana chana kadi yake ya uanachama hadharani jambo lililowaaudhi makada wa rais kwani ilikuwa inaonesha mgawanyiko katika chama huku uchaguzi mkuu ukisogea.
Inadaiwa kuwa Rais wa sasa Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kukipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC) na mpinzani wake mkuu Buhari.
Rais huyo wa zamani amekuwa mstari wa mbele kumkosoa rais wa sasa Goodluck Jonathan, ambaye anawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha PDP.
Kwa upande mwingine, Jeshi la Nigeria limemlaani Olusegun Obasanjo na kusema kuwa ameliabisha jeshi kwa kuashiria kuwa walikuwa na njama ya kuongeza muda.