Mwili wa Mtoto Mwenye ualbino wapatikana msituni
Mwili wa mtoto wa mwaka mmoja mwenye ulemavu wa ngozi Yohana Bahati aliyeporwa mikononi mwa mama yake juzi Mkoani Geita, umeonekana jana jioni ukiwa umekatwa miguu na mikono yote na kufukiwa ardhini kwenye hifadhi ya msitu wa Biharamulo, Wilayani Chato.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema mwili wa mtoto huyo umebainika jana majira ya saa 12:30 jioni ukiwa umefukiwa kwenye eneo ambalo linashamba la mahindi.
Mtoto mwingine mwenye ulemavu wa ngozi aliyeporwa mwezi desemba mwaka jana bado hajapatikana hadi leo licha ya jeshi la Polisi kungatangaza kutoa zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazo saidia kupatikana mtoto huyo.
Mauaji, ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi bado ni changamoto licha ya serikali kutafuta mbinu za aina mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuwapiga marufuku wapiga ramli.