Wednesday, 18 February 2015

Sera ya uhamiaji ya Rais Obama bado kitendawili

Sera ya uhamiaji ya Rais Obama bado kitendawili

Rais Barack Obama wa Marekani amesema hakubaliani na uamuzi wa jaji wa mahakama nchini humo wa kusitisha utekelezaji wa amri yake ya utendaji kuhusu mageuzi ya uhamiaji.
Akizungumza Ikulu ya nchi hiyo, Bwna Obama amesema sheria hiyo na historia viko upande wa utawala wake.
Wizara ya Usalama wa Ndani ya nchi imesema itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama na kwamba utawala umechukua mwelekeo mzuri kwa mujibu wa utawala wake wa sheria, lakini imeeleza kuwa kwa sasa itabidi ikubaliane na uamuzi wa mahakama.
Mageuzi ya Rais Obama kuhusu uhamiaji, yanatoa fursa kwa mamilioni ya wahamiaji wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria kutorejeshwa makwao.
Majimbo ishirini na sita ya Marekani yameomba kusitishwa kwa sheria ya rais huku hatua zaidi za kisheria kuufutilia mbali mpango huo wa rais zikiendelea.

clouds stream