Chenge awasilisha utetezi Baraza la Maadili, hatma yake kujulikana kesho
Aidha, Andrew Chenge miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni ya ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma na alipokuwa mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa Washauri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.
Ambapo ilielezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sheria.
Kufuatia tuhuma hizo , Chenge aliweza kujitetea kwa kuiwasilisha oda maalum ya utetezi wake dhidi ya madai anayodaiwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Maadili anayeshughulikia mashauri hayo Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema wataenda kukaa na kupitia oda hiyo ya Chenge na kisha watatoa maamuzi siku ya februari 26 mwaka huu ambayo ni kesho.
Katika hatua nyingine Baraza hilo la Maadili kesho litaendelea tena na shauri hilo la Chenge pamoja na viongozi wengine wa umma akiwemo aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.Anna Tibaijuka.