Tanzania yaporomoka kwenye viwango vya soka duniani
Takwimu zilizotolewa jana na FIFA zinaonesha kuwa Tanzania inashikilia nafasi ya 32 kwa upande wa Afrika.
Ivory Coast imepanda katika orodha ya shikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu. Kikosi cha Ivory Coast kimepanda nafasi nane juu hadi nafasi ya 20, lakini Algeria wanaendelea kuongoza kwa kuwa timu bora barani Afrika.
Mataifa kumi bora duniani barani Afrika: 1.Algeria 2.Ivory Coast 3. Ghana 4.Tunisia 5. Cape Verde 6.Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR
Mataifa kumi bora duniani: 1. Ujerumani 2. Argentina 3. Colombia 4. Ubeligiji 5. Uholanzi 6. Brazil 7. Ureno 8. Ufaransa 9. Uruguay 10. Hispania
Hakuna timu mpya iliyoingia wala kutoka kwenye orodha ya mataifa 10 duniani, hivyo kufanya orodha ya timu 10 bora duniani kubaki vilevile.