Majeshi ya UN nchini DRC.
Mashirika mbali mbali ya kiraia nchini
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba majeshi ya Umoja wa Mataifa
ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO kufikiria upya mpango wake
kujiondoa kupambana na kundi la waasi la FDLR.
Hapo jana majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika
operesheni hiyo kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo
serekali ya Kongo itakapotengua uteuzi wa majenerali wawili
walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo.
Kwa mujibu wa MUNUSCO majenerali hao wana tuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.