Thursday, 26 February 2015

Ligi kuu Ugiriki imesimamishwa kwa muda usio julikana

Ligi kuu Ugiriki imesimamishwa kwa muda usio julikana


Mchezo wa soka nchini Ugiriki umekuwa ukiandamwa na vurugu za mara kwa mara zitokanazo na mashabiki
Mchezo wa soka nchini Ugiriki umekuwa ukiandamwa na vurugu za mara kwa mara zitokanazo na mashabiki
Mechi za ligi kuu nchini Ugiriki zimeahirishwa kwa muda usiojulikana baada ya kutokea kwa vurugu kubwa.
Uamuzi huo umefikiwa na bodi ya ligi ‘Super ligi’ ya nchini Ugiriki baada ya kundi la mashabiki kuvamia uwanja kwenye mechi ya Athens ‘Derby’ mwishoni mwa wiki iliyopita, chama tawala cha Syriza kilicho chaguliwa hivi  karibuni kimedhamiria kudhibiti matatizo ya vurugu zitokanazo na mashabiki.
“Tumearifiwa kwamba Super ligi imesimamishwa kwa muda usiojulikana,” raisi wa Supa ligi Giorgos Borovilos amewaambia waandishi wa habari.
“Tuna serikali mpya sasa ambayo inatarajia kulileta swala hili kwenye majadiliano na utekelezaji wa kisheria utafuata kulingana na tatizo,” aliongeza.
Waziri wa michezo wa Ugiriki Stavros Kontonis amekutana na Waziri Mkuu Alexis Tsipras siku ya Jumatano iliyopita ili kujadili swala hilo na watakutana na Rais wa Super ligi Giorgos Borovilos.
Borovilos amesema bado haijajulikana mechi hizo zitasimamishwa kwa muda gani na kwa masharti gani, na akaongeza kuwa hakuna chochote kilichofanyika kwa muda wa wiki moja au mbili sasa.
“Serikali inataka mechi ziendelee haraka iwezekanavyo, lakini wanataka kuona hatua zikichukuliwa kutoka kwetu sote,” alisema Borovilos.
“Kutakua na majadiliano kati yetu, bodi ya Hellenic Football Federation (EPO) pamoja na ligi ya mpira wa miguu ambapo tutaona ni kwa jinsi gani tutaunda muundo wa ulinzi na sheria ili kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu unakua salama,” alisisitiza.
Hii ni mara ya tatu msimu huu kwa soka la kulipwa nchini Ugiriki kusimamishwa kwa sababu za vurugu.
Mechi zilisitishwa kwa wiki moja mwezi Septemba mwaka jana kufuatia kifo cha shabiki wa soka baada ya vurugu kwenye ligi daraja tatu kati ya Ethnikos Piraeus dhidi ya Irodotos.
Mamlaka zilisitisha michezo mwezi Novemba mwaka jana baada ya Christoforos Zografos, mkurugenzi saidizi wa kamati ya marefa wa kati (KED), alipo chukuliwa na kukimbizwa hospitali kufuatia kujeruhiwa kutokana na vurugu zilizo zuka uwnjani.

clouds stream