Urais 2015: CUF yamteua Prof. Lipumba kugombea urais
Kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha wananchi CUF Bwana Shaweji Mketo amesema kuwa kwa mujibu wa makubaliano na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi kila chama kitateua mgombea katika nafasi zote na kisha kushindanisha ili kupata mgombea moja atakayeungwa mkono na vyama vyote.
Ameongeza kuwa katika nafasi ya viti vya udiwani na ubunge kwa wanaotaka kugombea fomu zitaanza kutolewa kuanzia machi 1 hadi 10 kupitia makatibu wa matawi na katika nafasi ya ubunge wagombea watatakiwa kuchukua fomu kwa makatibu kata na kuzirudisha kwa makatibu wa wilaya.
Katika hatua nyingine amesisitiza kuwa aprili 17 hadi 19 kurugenzi ya uchaguzi inatarajia kukaa na kufanya mchujo kwa wagombea ubunge