Rais Kikwete ateua wakuu wa Wilaya wapya 27
\
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA
27, Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42
kwenye vituo vyao vya zamani.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko
ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya
kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya
zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na
kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu
kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa
majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu
wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais
Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza
kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni
Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike
anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda
Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred
Mwakalebela anayeenda wilaya ya Wanging
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni
Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali
Kimiang;ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni),
Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S.
Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara
(Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen
Zelothe (Musoma)
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud
A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack
(Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo
Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally
Mohamed (Serengeti)
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao
umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas
Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa
Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa
Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa
Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa
Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri,
kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa
ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred
Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo
Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses
Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya
(Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias
Goroi (Rorya)