Watu 22 wafariki kwenye uwanja wa michezo nchini Misri
Misri imesimamisha ligi ya soka nchini humo baada ya vurugu za mashabiki kwenye mechi ya ligi hiyo kati ya Zamarek na ENPPI, kwenye tukio hilo ambalo ni kama la 2012 ambalo watu zaidi ya 74 walifariki dunia kutokana na matatizo viwanjani yanayokumba sana soka la Misri.
Tukio hilo limetokea baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.Polisi wamesema mashabiki hao walikuwa wanataka kuingia uwanjani bila tiketi, wamenukuliwa wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi kutokana na msongamano mkubwa wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.
Ndani ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili ya Watu waliopoteza maisha na wengine waliolala wakiwa majeruhi.