Afrika kusini: Ngumi zapigwa Bungeni, upinzani watimuliwa
Sakata hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la kifahari la Nkandla.
Kwa upande mwingine Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameingia kwenye kashfa ya ufujaji wa fedha za Serikali yake kutokana na kufanya ukarabati wa jumba lake la kifahari kwa gharama ya dola milioni 25 sawa na zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania.
Taarifa za nchini humo zinaeleza kuwa, ukarabati huo wa jumba lake gharama zake zote zinatarajiwa kulipwa na serikali. Kufuatia hatua hiyo, uchunguzi umeanza kuhusu ukarabati huo ambao ni nyumba yake binafsi na sio mali ya umma.