Akuffour anyolewa nywele baada ya Ghana kupigwa kwenye fainali

Mchezaji wa zamani wa timu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ghana akinyolewa nywele jana baada ya Ghana kufungwa
Akuffour alitabiri kuwa Ghana wangeibuka na ushindi katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast na kama wasiposhinda basi anyolewe nywele zake.
“Mleteni kabisa kinyozi kwenye jumba hili kubwa, ili Ivory Coast wakishinda aninyoe nywele zangu zote,” Akuffour alisema kabla ya mechi kuanza.
Na baada ya mechi kumalizika na Ivory Coast kushinda kwa penati 9-8 dhidi ya Ghana ndipo mtangazaji mmoja akachukua mashine ya kunyolea na kuanza kunyoa Akuffour.