Shida ya maji yawatesa wananchi Shinyanga
Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wanaendelea kuteseka kufuatia kukosa huduma ya maji safi ikiwa ni mfululizo wa siku nne.
Aidha, tatizo la ukosefu maji limetokana na mitambo ya kusukuma maji kutoka chanzo cha ziwa Victoria (Ihelele), na kusambaza maji hayo katika miji ya Kahama na Shinyanga kupata hitilafu kwenye mfumo wa umeme.
Wakizungumza na mwandishi wa Habari wa Mtandao wa Hivisasa wananchi wa manispaa hiyo wametupia lawama mamlaka za kusambaza maji za mji wa kahama na Shinyanga (KASHUWASA) pamoja na Mamlaka ya maji safi na maji taka ya mji wa Shinynga (SHUWASA) kwa kushindwa kutatua tatizo hilo kwa wakati.
Mwandishi wetu ameshuhudia msululu wa wananchi wakihaha katika maeneo mbalimbali kutafuta maji suala linalopelekea washindwe kujikita katika shughuli nyingine za kukuza uchumi wao.