Raia 13 wa Ethiopia wafikishwa mahakamani kwa kukiuka sheria
Zaidi ya raia 13 wa Ethiopia wanashikiliwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kuvunja sheria za nchi kwa kuishi Tanzania bila kuwa na vibali maalum vya kuishi nchini.
Aidha, Jaji anayehusika na matatizo ya uhamiaji haramu kwenye mahakama ya Kisutu Jaji Emmillius Mchauru amesema watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Feb 6, 2015 na raia wote wamekiri makosa hayo isipokuwa mtuhumiwa mmoja Bw. Anamo Yohanes ambaye wakati wenzake wakiwa mahakamani yeye alikuwa Hospitalini.
Watuhumiwa hao waliokutwa na matatizo hayo mnamo Feb 6,2015 na walienda kwa majina ya Melkamu Molore, 18, Adenew Dana, 19, Tefera Mishamo, 20, Redwan Hussein, 18, Anamo Yohanes, 19, Mohamad Samawi, 18, Tegetel Regiso,20, Tegotoe Tarafa, 26, Eligudo Butiro, 18, Bahiradina Abule, 19, Desta Chafamu, 20, Marcus Dawye, 20, na Tashala Matiko, 20.
Kesi hiyo imesogezwa mpaka Feb 24 na kama ikidhibitishwa makosa yao watawekwa ndani kwa kuvunja sheria ya nchi ya kuingia na kuishi nchini bila kuwa na vibali.