Kluivert awapiga msasa Stand United

Mchezaji
wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick
Kluivert (wa tatu kutoka kushoto) akizungumza na wandishi wa habari
Mafunzo hayo kwa klabu ya Stand United, aliyafanya kabla ya kufungua kituo cha michezo kwenye shule ya Sekondarin ya Com. Kluivert alifungua kituo cha michezo katika shule ya sekondari Com ambapo aliambatana na mwenyeji wake Steven Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga na ni Naibu Waziri wa wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais.
Kluivet amewashauri wachezaji wa Stand United kuwasikiliza walimu wao na kuzingatia vitu wanavyofundishw na walimu wao, pia akasema ni lazima watambue kua wanafanya nini na wasimamie malengo yao.
“Katika kucheza mpira, mchezaji yeyote anatakiwa kuwa na vitu vitatu muhimu kwanza anatakiwa awe na nidhamu, awe msikivu kwa mwalimu wake na kujituma katika mazoezi. Akifanya hivyo lazima atafanya vizuri.” Kluivert alisema.
Kluivert alitoa mbinu mbalimbali za kufunga kwa urahisi, lkini pia akafundisha jishi ya kujilinda na mashambulizi ya timu pinzani.