Mtoto mwingine mwenye ualbino atekwa nyara Geita
Maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino nchini Tanzania yanaendelea kuwa mashakani kufuatia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino kutekwa katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani humo limesema kuwa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja alitekwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana jana usiku.
Habari zinasema watu waliokuwa na silaha za jadi waliwaweka chini ya ulinzi Bahati Misalaba na mkewe ambao ni wazazi wa mtoto albino ambaye walimteka na kutoweka naye.
Familia hiyo pia ina watoto wengine wawili wenye ulemavu wa ngozi, Tabu Bahati mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja ambao walinusurika kuchukuliwa na watu hao kwa sababu wakati unyama huo ukitendeka nyumbani kwao hawakuwepo walikwenda kucheza kwa majirani zao.
Inadaiwa kuwa Mama wa mtoto huyo alijeruhiwa vibaya wakati akimpigania mtoto wake asichukuliwe na watu hao.
Matukio ya ukatili dhidi ya alino yamesambaa katika mikoa yak kanda ya ziwa huku imani za kishirikina ikidaiwa ndiyo sababu kubwa inayaosababisha utekaji na mauaji kwa watu wenye ualbino.
Kufuatia tukio hilo Jeshi polisi limeanza msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.