Ngassa: Yanga inanitesa na deni
Winga wa Yanga Mrisho Ngassa amesema mara baada ya kujiunga na klabu ya Yanga akitokea Simba SC alikokua anakipiga kwa mkopo kuulibuka deni la Sh. Milioni 45 alilotakiwa kuilipa klabu ya Simba, ikiwa ni agizo la TFF kwa sababu mchezaji huyo alisaini kujiunga na Yanga wakati alikua bado anamkataba halali na klabu ya Simba.
Klabu ya Yanga ilimshauri Ngassaachukue mkopo ili alipe deni hilo kitu ambacho Ngassa anasema alikigomea katika hatua za awali, lakini uongozi wa Yanga ukaahidi kumsaidia kulipa deni hilo.
“Sikua tayari kusaini mkopo ule, niligoma kabisa lakini wakanilazimisha wakaniahidi kwamba klabu nayo itanisaidia kulipa lakini baadae mambo hayakua hivyo, niliendelea kukatwa pekeangu,” alisema Ngassa.
Kunakipindi ambacho wakati nakatwa hizo fedha kumbe zilikua hazifiki benki, sikua najua zilikokua zinapelekwa lakini zilikua zinakatwa kwenye mshahara wangu na mimi kuendelea kupata mshahara kiduchu,” Ngassa alilalamika.
Hadi Ngassa sasa amefunga magoli mawili tu kwenye ligi msimu huu, lakini mwaka jana aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champions League), ameitaka Yanga kumsaidia kulipa deni lake ili aweze kucheza soka la kutakata kwa moyo mmoja.
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Jerry Murro amesema kwamba klabu ya Yanga haina mgogoro wowote na mchezaji huyo na tayari wameanza mazunguzo ya kuongeza mkataba.