Mbunge, walinzi wake wauawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Nairobi Kati OCPD Paul Wanjama amesema katika tukio hilo walinzi wawili wa Mbunge huyo na dereva nao wameauawa kwa kupigwa risasi.
Akizungumzia tukio hilo dereva aliyeshuhudia tukio hilo alisema kwamba gari la mbunge huyo lilisimama katika eneo la Mzunguko (roundabout) ambapo watu nne walitokea wakiwa na bunduki na kuanza kuwashambulia.
Ameongeza kuwa waliwamininia risasi nyingi na hatimaye kutoweka. Baada ya muda walifika katika eneo la tukio ambapo mbunge huyo akiwa na wenzake tayari walikuwa wameuawa.
Naye muuza magezeti aliyeshuhudia tukio hilo aliwaambia Polisi kuwa mmoja wa wauaji hao alikuwa amejifunika usoni (mask). Miili ya Mbunge na pamoja na walinzi walio uawa imeonekana kuwa na matundu ya risasi kichwani pamoja na kifuani ambapo imepelekwa katika maeneo ya Lee nchini Kenya.
Katika hatua nyingine Seneta wa Kiambu Bw. Kimani Watamangi amesema Bw. Muchai alikuwa anatishiwa mara kadhaa na aliwahi kuripoti katika jeshi la Polisi nchini humo.