Tuesday, 24 February 2015

Barcelona, Juventus zatamba ligi ya mabingwa Ulaya

Barcelona, Juventus zatamba ligi ya mabingwa Ulaya


Mshambuliaji wa FC Barcelona Luis Suarez kifunga goli la kwanza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester City
Mshambuliaji wa FC Barcelona Luis Suarez kifunga goli la kwanza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester City
Manchester City ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Etihad imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Barcelona katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Luis Suarez alifunga magoli yote mawili kwa upande wa Barcelona katika dakika ya 16 na 30 akipokea pasi za mwisho kutoka kwa Jord Alba wakati Sergio Aguero ameifunga City bao la kufutia machozi katika dakika ya 69 akimalizia pasi ya David Silva.
Dakika ya 74 mlinzi wa Manchester City, Gael Clichy alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano. Nyota wa Barcelona Lionel Messi amekosa penalti dakika ya 90 baada ya mlinda mlango Joe Hart kupangua mkwaju huo.
Katika mchezo mwingine uliopigwa Italia, Juventus imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Juventus Stadium kuwaadhibu Borrusia Dortmundkwa goli 2-1 katika mchezo wao wa kwanza.
Carlos Tevez aliifungia Juventus goli la kuongoza katika dakika ya 13, lakini Marco Reus alisawazisha dakika tano baadaye.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Alvaro Morata aliandika bao la pili lililoduma mpaka dakika 90 ya mchezo.
Timu hizo zitacheza mechi za marudiano majuma mawili yajayo ili kuamua nani atasonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.

clouds stream