Thursday, 30 June 2016

Fimbo Yapoteza Maisha Ya Askari Wa JWTZ


Tarehe July 1, 2016fimbo
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikosi cha 212 kilichopo Milambo mkoani Tabora, ameuawa kwa kipigo kutoka kwa wafugaji akiwa eneo lake la ujenzi.
Aliyeuawa katika tukio hilo katika kijiji cha Usule kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora ni Crius Mkumozi mwenye umri wa miaka 35.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo inadaiwa alikuwa akichunga mifugo kwenye eneo la askari huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa amesema askari huyo alipigwa fimbo kichwani na begani baada ya kujaribu kuondoa ng’ombe waliokuwa kwenye eneo lake.
Kamanda Issa amesema mtuhumiwa ambaye hakutaka kutaja jina lake, anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.

Kocha Omog Kusaini mkataba na simba Leo

Tarehe July 1, 2016
Joseph OmogJoseph Omog
Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog anatarajiwa kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Simba kabla ya kusaini Mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha klabu hiyo.
Omog na Simba SC wamefikia makubaliano baada ya mazungumzo ya awali kwa njia ya simu na barua pepe na Mcameroon huyo amekubali kuja kusaini Mkataba Dar es Salaam baada ya kutumiwa tiketi.
Simba itakuwa klabu ya pili kwa Omog kufundisha Tanzania baada ya awali kuwa na Azam FC, aliyoiongoza kwa msimu mmoja na nusu ikishinda mechi 30 kati ya 55 za mashindano yote, sare 14 na kufungwa 11.

Ukawa Watinga Bungeni Na Nguo Za ‘Msiba’, Mabango


Tarehe June 30, 2016Untitled
Untitled
Baadhi ya wabunge wanaotoka vyama vya siasa wakiwa nje ya ukumbi wa bunge baada ya kususia kikao cha bunge leo
Wabunge wa Kambi ya Upinzani leo wametoka nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa na mabango mbalimbali yenye ujumbe wa kwenda kwa Rais Dkt John Magufuli na Naibu Spika Ackson Tulia.
Kabla ya kutoka nje, wabunge hao waliokuwa wamevalia mavazi yenye rangi nyeusi walisimama ndani ya ukumbi wa bunge kwa dakika chache huku wakiwa wamenyanyua mabango yao juu.
Huu ni muendelezo wa wabunge wa upinzani kususia vikao vinavyoendeshwa na naibu spika, Dkt Tulia wakidai kuwa amekuwa akikiuka kanuni za uendeshaji wa bunge.

Safari Ya NEC Dodoma Yaanza Kunukia


Tarehe June 30, 2016Lubuva+PHOTO
Lubuva+PHOTO
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutekeleza agizo la Rais Dkt John Magufuli la kujenga Ofisi Kuu ya Tumemjini Dodoma baada ya jana kuoneshwa kiwanja katika eneo la Iyumbu katika Manispaa ya Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema katika uchaguzi zijazo wataanza shughuli za usimamizi wakiwa Dodoma.
“Katika Uchaguzi Mkuu ujao, wapambe wa wagombea watakaa nje ya viwanja hivi wakiwasubiri watu wao wachukue fomu, huu ni mwanzo wa safari yetu ya kuhamia rasmi mjini Dodoma,” alisema Jaji Lubuva akionesha kiwanja hicho ambacho kimenunuliwa kutoka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).
Akizungumza baada ya kukagua eneo la ekari 10 litakalotumika kujenga ofisi hizo, Lubuva alisema huo ni mwanzo wa safari ya kuhamia Dodoma na kwamba tume ilikuwa na lengo la kuwa na jengo la kutosheleza mahitaji kwa muda mrefu  kwani sasa ofisi ya tume hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam ina ofisi tatu maeneo matatu tofauti.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani alisema eneo hilo lina miundombinu yote na wameanza mazungumzo la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili ifikapo Oktoba ujenzi uanze na baada ya mwaka mmoja tume iwe na jengo lake.

Magufuli:Tumemkamata Mwizi Wa Milioni 7 Kila Dakika


Tarehe June 30, 2016Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amewaacha wananchi midomo wazi kufuatia kauli yake kwamba serikali imemkamata mtu aliyekuwa akiibia Mamlaka ya Mapato kiasi cha shilingi milioni 7 kila dakika.
Aidha,Rais Magufuli alisema hayo  wakati  akiwaapisha  na kula kiapo cha uadilifu wakuu wa Mikoa wapya na wakuu wa wilaya Ikulu jijini Dar es salaam.
“Yuko mtu mmoja alikuwa anafanya transaction ya fedha kila dk 1 kati ya milioni 7 na 8. Serikali ilikuwa inapoteza pesa, bahati nzuri huyo mtu yuko mikono salama, tunatafuta jinsi ya kuzirudisha’”Alisema Rais Magufuli.
Hata hivyo mkuu huyo wa nchi hakuweza kufafanua zaidi kuhusu mtu huyo ambaye bila shaka atakuwa ni  Bilionea kutokana na kuiibia serikali fedha hizo kila dakika ambazo ni jasho la wananchi wanaolipa kodi.

Wednesday, 29 June 2016

NBS Yakana Kupima UKIMWI Nyumba Kwa Nyumba


Tarehe June 29, 2016BARAZA-1-620x309
BARAZA-1-620x309
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kwamba, ugonjwa wa Ukimwi sasa utapimwa nyumba kwa nyumba.
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo imesema, habari hizo zinatokana na taarifa iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la tarehe 24 Juni, 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari “Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba”.
NBS imefafanua kuwa ofisi hiyo itafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania kuanzia Septemba 2016 ambapo Ukimwi utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huu.
Utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.
Aidha, katika utafiti huu kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo.

Ripoti Ya Lugumi Kuwasilishwa Bunge Lijalo


Tarehe June 29, 2016aeshy
aeshy
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi
Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano wa bunge unaoendelea, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.
Sakata hilo linahusisha utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.
Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.
Baada ya sakata hilo kuibuliwa, wabunge walitaka liwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea mjini Dodoma, lakini PAC ikaunda kamati ndogo ambayo sasa inatakiwa iwasilishe ripoti ya uchunguzi wake.
Hadi jana asubuhi ripoti ya kamati hiyo ndogo, iliyoundwa na wajumbe tisa, ilikuwa bado haijawasilisha ripoti yao.

‘Tanzania Haitaathirika Uingereza Kujitoa EU’


Tarehe June 29, 2016MELROSEDIANA
Balozi wa nchi Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose
Siku chache baada ya Uingereza kuamua kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), Balozi wa nchi hiyo nchini, Dianna Melrose amesema wataendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania ili kuhakikisha uwekezaji haupungui.
Akijibu swali kuhusu athari zozote zitakazojitokeza kwa Tanzania baada ya Uingereza kujitoa EU, Balozi huyo alisema kuwa suala hilo haitapunguza uwekezaji, misaada wala vita dhidi ya rushwa na uhalifu wa kimtandao.
“Uhusiano wetu utaendelea kuwa imara kama ulivyokuwa awali,” alisema Melrose.
Tangu Juni 23 Uingereza ilipopiga kura ya maoni kujitoa EU, umetokea mtikisiko mkubwa kati ya Uingereza na washirika wake Wales, Scotland na Ireland Kaskazini, huku hali hiyo ikihofiwa kuweza kuathiri nchi ambazo zina wawekezaji kutoka Uingereza.
Balozi Melrose alisisitiza kuwa Uingereza itaendelea kuwa mwanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato), Umoja wa nchi saba zilizoendelea zaidi duniani (G7), umoja wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani (G20) na Jumuiya ya Madola na kushirikiana na Tanzania.

Tuesday, 28 June 2016

Hispania yavuliwa ubingwa

Timu ya taifa ya hispania imeaga michuano ya ulaya baada ya kufungwa na timu ya italia kwa jumla ya mabao mawili bila majibu. Timu ya Hispania ambayo ndio ilikuwa bingwa mtetezi imeaga michuano ya ulaya 2016. Katika mechi hii timu zote mbili zilikuwa zinagombani nafasi ya kucheza robo fainali ya kumbe la ulaya.  Katika dakika ya 33 timu ya Italy ilijipatia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake mahiri Giogrio Chiellini baada ya kipa wa Hispania, De gea kucheza mpira wa adhabu uliopigwa na kisha mchezaji Giogrio Chiellini kuumalizia.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya italia ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao moja. Kipindi cha pili kilianza huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

 Lakini katika dakika za lala salama mchezaji Graziano Pelle wa italia aliifungia timu yake ya italia bao la pili, dakika ya 90. Hadi mwisho wa mchezo refa Cuneyt Cakir alipopuliza kipenga cha mwisho, Italia ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.


clouds stream