Tuesday, 31 October 2017

Nape Akana Taarifa Iliyozagaa Mitandaoni



Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.

Baada ya Mbunge Lazaro Nyalandu kujiuzulu na kuhamia chama cha Chadema,Nape amekana taarifa iliyoenea mitandaoni kuwaatazungumza na  Waandishi wa Habari leo.

Kupitia ukurasa wake wa Mitandao ya kijamii Nape amesema hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema
kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

“Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina ‘press conference’
kesho” aliandika Nape Nnauye.

Zitto Kabwe Akamatwa Na Polisi Dar


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe.


Hatimaye, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe, amekamatwa na Jeshi la Polisi asubuhi hii akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam na amepelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Hayo yameibanishwa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis ambapo amesema sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaamkatika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini.

Hivi karibuni Zitto kabwe amekua akikosoa serikali kuhusiana na hali ya uchumi wa nchi kukua suala ambalo Zitto amesema
haliendani na uhalisia wa maisha ya wananchi

Kenyatta atangazwa mshindi wa urais Kenya akiwa na kura 7.5m

 Uhuru KenyattaRaisi Uhuru Kenyata

Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi wa urais wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati amesema kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.

Bw Chebukati amesema jumla ya wapiga kura 7,616,217 kati ya jumla ya wapiga kura 19.6 milioni ambao wamejiandikisha kuwa wapiga kura nchini humo walishiriki uchaguzi huo wa Alhamisi wiki iliyopita.

Hiyo ni asilimia 38.84.

Rais Kenyatta, akihutubu baada ya kutangazwa mshindi, amewashukuru waliompigia kura.

Amesema uchaguzi uliomalizika ni ishara ya uthabiti wa demokrasia na uthabiti wa taasisi za Kenya pamoja na Wakenya wenyewe.

"Agosti 8, na sitachoka, Wakenya walirauka kupiga kura. Na siku hiyo walinichagua bila shaka. Ushindi wangu ulipopingwa Mahakama ya Juu, kwenye hukumu, mahakama haikupinga ushindi wangu wa 54%. Takwimu hazikupingwa. Kilichokosolewa ni utaratibu uliopelekea ushindi wangu," amesema.

Bw Odinga alikuwa ametarajiwa kutangaza mwelekeo kwa wafuasi wake baada ya tangazo la matokeo kufanywa na Bw Chebukati.

Taarifa zinasema ameamua kufanya hivyo hapo kesho.

Matokeo kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati

MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee7,483,89598.28
Raila Odinga (Alisusia)ODM73,2280.96
Mohamed Abduba DidaARK14,1070.19
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea8,2610.11
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea6,0070.08
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea5,5540.07
John Ekuru AukotThirdway Alliance21,3330.28
Cyrus JirongoUDP3,8320.05

Bw Chebukati amesema anaamini uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.

Mwenyekiti huyo amesema mambo aliyosema yalihitajika kufanyika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki yalitimizwa.

Amesema walitaka kuhakikisha kila kitu kilikuwa sawa.

"Hata tulibadilisha tarehe kutoka 17 hadi 26 Oktoba kuhakikisha tuna muda wa kutosha," amesema.

Kadhalika, amesema alikuwa na kundi la kusimamia mradi wa uchaguzi wa urais kuondoa majukumu kutoka kwa makamishna ambao walituhumiwa na baadhi ya wadau.

"Naweza kusema kwa uhakika, kwamba 26 Oktoba kabla ya uchaguzi kuanza, nilikuwa nimeridhika kwamba tulikuwa tumefanya kila kitu kuhakikisha kila Mkenya angetekeleza haki yake kikatiba," amesema.

"Na haki hii mtu anafaa kuitekeleza bila kutishiwa au kuzuiwa."

Bw Chebukati anasema alishangaa kwamba watu waliotafuta wa kushambulia walimwendea yeye.

Hata hivyo, anasema ndani ya tume nao walimwogopa.

"Hatutaweza kufurahisa kila mtu. Nimedumisha na kuheshimu sheria, kama mwanasheria ziwezi kuvunja sheria niliyojitolea kuilinda," amesema.

Matokeo yalivyokuwa uchaguzi wa tarehe 8 Agosti ambao ulifutwa na Mahakama ya Juu

MgombeaChamaKuraAsilimia
Uhuru KenyattaJubilee8,203,29054.27
Raila OdingaODM6,762,22444.74
Mohamed Abduba DidaARK38,0930.25
Japheth Kavinga KaluyuMgombea wa kujitegemea16,4820.08
Michael Wainaina MwauraMgombea wa kujitegemea13,2570.09
Joseph Nthiga NyagahMgombea wa kujitegemea42,2590.28
John Ekuru AukotThirdway Alliance27,3110.18
Cyrus JirongoUDP11,7050.08

Monday, 30 October 2017

Mbunge wa CCM Lazaro Nyalandu ajiuzulu Tanzania

Bw Nyalandu

Mbunge wa chama tawala nchini Tanzania CCM Lazaro Nyalandu amejiuzulu wadhifa wake, na kusema kwamba anataka kuhamia chama cha upinzani Chadema.

Bw Nyalandu, Aliyekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii wakati wa serikali ya awamu ya Tano nchini Tanzania amesema kupitia taarifa kwamba amejuzulu nyadhifa zake zote ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo ubunge.

Nyalandu ambaye kabla ya maamuzi hayo ya kujiuzulu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama.

Katika taarifa yake ya kujiuzulu aliyoiweka katika ukurasa wake wa Facebook, Nyalandu amesisitiza umuhimu wa nchi hiyo kupata katiba mpya.

"Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali," amesema.

"Nimemua kujiuzulu Kiti cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania.

"Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo."

Nyalandu anaingia katika orodha ya mkururu wa viongozi wa juu wa CCM waliokihama chama hicho na kuhamia chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema tangu mwaka 2015.

RAIS MAGUFULI APONGEZA MABADILIKO CUF



Daraja la Furahisha



Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaunga mkono mabadiliko yanayotokea katika Chama cha Wananchi (CUF) na kupongeza hatua hiyo.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa daraja la Furahisha litakalotumiwa na waenda kwa miguuMkoani humo.

Akikamilisha hotuba yake na kumtambua Mbunge wa Liwaled, Mhe. Zuberi Kuchauka (CUF), Rais Magufuli amesema wanawapongeza CUF kwa mabadiliko wanayofanya na kumtaka mbunge huyo kufikisha salamu zake na pongezi nyingi kwa mabadiliko hayo.

“Tunawapongeza sana kwa mabadiliko mnayofanya na ukawafikishie salamu zetu,” amesema Rais Magufuli.

Awali mbunge huyo alipopewa nafasi ya kusema machache, alimmiminia sifa nyingi Rais Magufuli na kumuombea dua ili awe na afya njema aweze kutimiza lengo lake na kukuza viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati.

“Mhe. Rais, sisi sote tunatambua kazi nzuri unayoifanya ya kuwaletea maendeleo Watanzania na mimi napenda nikupongeze sana kwa hilo na ndiyo maana nakuombea dua uzidi kuwa na afya njema,” amesema.

Hivi karibuni CUF imekuwa katika hekaheka na migogoro isiyokwisha na kupelekea chama hicho kupasuka vipande viwili, ambapo upande mmoja unaamini katika CUF ya Mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba huku upande wa pili ukiwa unaamini katika CUF ijulikanayo kama CUF Maalim, ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF.

NECTA YAONYA WANAFUNZI WASIMAMIZI MTIHANI WA KIDATO CHA NNE UKIANZA LEO

Image result for wanafunzi

Wanafunzi katika moja ya shule ya sekondari nchini.



Baraza la Mtihani nchini (NECTA) limesema halitosita kumchukulia hatua mwanafunzi yeyote pamoja wasimamizi wa Mitihani hiyo
ambao watakiuka sheria za mitihani ya kidato cha nne ambayo inaanza leo saa mbili za asubuhi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa (NECTA), Dkt Charles Msonde wakati wa mkutano na waandishi, ambapo amesema
Baraza hilo linatoa wito kwa kwa wasimamizi wa mitihani wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu.

“Tunawaasa wasimamizi wa mitihani pamoja na wanafunzi kujiepesha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatuakali kwa yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya Taifa” amesema Dkt Msonde.

Amesema Baraza hilo linawataka wamiliki wa shule kutambua kuwa shule zao ni vituo maalum vya mitihani na hivyo havitakiwi
kuingilia majukumu ya wasimamizi.

Aidha,katika mitihani huo jumla ya watahiniwa 585,938 wamesajiliwa kufanya mtihani huo, ambapo kati yao watahiniwa wa shule ni 323,513 na watahiniwa wa kujitegemea ni 62,425.

“Kati ya watahiniwa wa shule 323,513 waliosajiliwa ,wanaume ni 159.103 sawa na asilimia 49.18 na wanawake ni 164,410 sawa
na asilimia 50.82,huku watahiniwa wenye uono hafifu ni 305 ambapo maandishi yao yanakuzwa”amesema Dkt Msonde.


Friday, 27 October 2017

JAHAZI LAKAMATWA LIKISAFIRISHA HEROIN YA BILIONI 5




Dawa za kulevya aina ya Heroini.



Maofisa wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) wakishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wamekamata zaidi ya kilo 100 za madawa ya kulevya aina ya Heroin zenye thamani ya Shilingi bilioni 5 zilizokuwa zikisafirishwa kwenye jahazi kutoka Unguja kwenda Dar es Salaam.

Kamishna wa Sheria wa DCEA, Edwin Kakolaki amesema hatua hiyo ilifikiwa baada ya maofisa hao kutilia shaka jahazi hilo ambalo ndani yake lilikuwa na raia kumi wa Iran na Wazanzibari wawili.
“Paketi 104 za madawa ya kulevya yanayoshukiwa kuwa ni heroin zilikamatwa katika jahazi hilo na kupelekwa kwa Mkemia Mkuuwa Serikali kwa vipimo zaidi,” amesema.

Amesema hadi jana jioni walikuwa wamefanya upekuzi kwa kusaidiana na mbwa maalum wa kunusa ili kuona kama kuna mzigo zaidi katika jahazi hilo.

Naye Kamishna Mkuu wa DCEA, Rodgers Siang’a amesema kiwango cha dawa hizo kingekuwa kikubwa zaidi kama sio kitendo cha watu hao kutupa kiasi kingine baharini baada ya kuzidiwa nguvu walipozungukwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Vyombo vya dola viko imara kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya na hatutaacha kuyadhibiti magenge na mitandao yao,” amesema Siang’a.

Hatahivyo, upekuzi huo haukukamilika kutokana na hali ya mvua ambapo unatarajiwa kuendelea leo huku taratibu za kwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali zikikamailika, watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani.

Rais Magufuli Apangua Wakuu Wa Mikoa,Makatibu Wakuu




Rais Dkt.John Pombe Magufuli.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo.

Majina ya waliteuliwa yametangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ambapo amesema walioteuliwa ni Wakuu wa
mikoa, Makatibu Wakuu, na Manaibu Katibu Wakuu.

Tuesday, 24 October 2017

Buffon achukua nafasi ya Neuer kikosi bora cha Fifa

Gianluigi Buffon


Gianluigi Buffon ameshinda Serie A mara kumi



Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza kikosi bora cha soka ya wanaume duniani mwaka 2017 ambapo kuna mabadiliko matatu kutoka kwa kikosi kilichotangazwa mwaka 2016.

Kwenye kikosi hicho, maarufu kama Fifpro World XI, mlindalango Gianluigi Buffon amechukua nafasi ya Manuel Neuer, naye beki wa AC Milan Leonardo Bonucci akachukua nafasi ya kigogo wa Barcelona Gerard Pique kwenye safu ya ulinzi.

Mshambuliaji wa PSG Neymar, ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani naye ameingia nafasi ya Luis Suarez katika safu ya mashambulizi.

Kikosi hicho kina wachezaji watano kutoka Real Madrid, wawili wa Barcelona, wawili wa PSG, mmoja wa Juventus na mmoja kutoka AC Milan.

Hakuna mchezaji hata mmoja wa Ligi ya Premia aliyefanikiwa kujumuishwa katika kikosi hicho.

Fifpro World XI

Mkufunzi bora duniani soka ya wanaume

Zinedine Zidane amemshinda meneja wa Chelsea Antonio Conte baada ya kuongoza Real Madrid kushinda La Liga msimu uliopita kwa mara ya kwanza tangu 2012 na kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia msimu uliopita.

Conte alishinda Ligi ya Premia msimu uliopita.
Massimiliano Allegri wa Juventus, ambaye aliongoza klabu yake kushinda Serie A na Coppa Italia msimu uliopita alikuwa wa tatu.

Mkufunzi bora soka ya wanaume
Zinedine Zidane - 46.22%Antonio Conte - 11.62%Massimiliano Allegri - 8.78%

Mkufunzi bora duniani soka ya wanawake

Kocha wa Uholanzi Wiegman aliyeongoza Uholanzi kushinda Euro 2017 nyumbani kwao amechukua taji hilo.Waliwalaza Denmark kwenye fainali.

Sarina Wiegman akipokea taji lake
Sarina Wiegman akipokea taji lake

Mkufunzi bora wa soka ya wanawake
Sarina Wiegman - 36.24%Nils Nielsen - 12.64%Gerard Precheur - 9.37%
   

Kipa bora zaidi

Mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa Serie A mara 10 Gianluigi Buffon ndiye mshindi wa tuzo ya mlindalango bora duniani mwaka huu.

Aliwasaidia Juventus kushinda taji la ligi mara ya sita mtawalia msimu uliopita.
Aidha, alicheza dakika 600 Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya bila kufungwa.

Buffon, 39, amewashinda kipa Keylor Navas, wa Real Madrid na Manuel Neuer wa Bayern Munich.
"Ni heshima kubwa sana kwangu kupokea tuzo hii katika umri wangu huu," alisema Buffon.

Uchezaji haki

Mchezaji wa Togo Francis Kone, ambaye alimfanyia huduma ya dharura kipa wa Bohemians 1905 Martin Berkovec uwanjani wakati wa mechi ya ligi Jamhuri ya Czech mwezi Februari ametunukiwa tuzo ya uchezaji wa haki.

Afande Sele Ammwagia Makonda Sifa Lukuki Kwa Hili, Adai Mengine Hayamuhusu






Msanii Mkongwe wa Muziki wa Hip Hop, Afande Sele ameibuka na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makondakwa kitendo chake cha kuyakusanya magari mabovu ya askari na kwenda kuyakarabati.

Rapa huyo amesema kitendo cha mkuu huyo kimeonyesha taswira tofauti na kusema kuwa zamanimagari ambayo yalikuwayanachakaa yalikuwa yanauzwa kwa watumishi wa jeshi hilo kwa bei ya kutupa lakini yeye ameamua kufanya tofauti.

“Ingekuwa zile siku za zamani kidogo haya magari aliyoyakarabati huyu mkaka wa Dar wangeuziana mabosi wapolisi na wapendwa wao kwa shilingi laki mbili kila moja kama vyuma chakavu,” ameandika Afande Sele katikaukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

“Katika hili huyu jamaa wa Dar anastahili kongole lakini yale mengine mimi hayanihusu bora nikae kimya kwanzakwetu sio Dar,” ameongeza Afande Sele.

Mhe. Makonda hivi karibuni alikabidhi magari ya kisasa 18 kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,Lazaro Mambosasa kwa ajili ya kusaidia kupambana na uhalifu na kuimarisha ulinzi na usalama katika Jiji la Dar es Salaam.

Magari hayo ni kati ya yale 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa mabovu kwaajili ya kufufuliwa upya.

GAVANA MPYA WA BOT AFUNGUKA AAHIDI HAYA






Gavana Mteule wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema kuwa amepokea kwa heshima kubwa dhamana aliyopewa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na anatambua changamoto za nafasi hiyo.

Profesa Luoga ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – Taaluma, amesema kuwa atatumia
wataalamu wa BoT kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa huku akihitaji ushirikiano wa kila mtu katika kufanikisha kazi aliyopewa.

“Nimepokea kwa heshima dhamana niliyopewa nikitambua kwamba zipo changamoto. Nitakwenda kujifunza zaidi kwa sababu sijawahi kuwa Gavana, nitatumia wataalamu waliopo katika kutekeleza majukumu yangu,” amesema Profesa Luoga.

Rais Magufuli Julai 11,2017 alimteua Profesa Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Novemba mwaka jana na bodi hiyo kuvunjwa.

Profesa Luoga ni mtaalamu katika masuala ya sheria za kodi na amefundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1986 kabla ya kupandishwa cheo na kuwa profesa mshiriki (Associate Professor) mwaka 2005.

Ameshika nafasi mbalimbali chuoni hapo ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Misaada ya Kisheria katika Kitivo cha Sheriamwaka 1993 – 1995, Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada za Awali (2005 – 2009), Katibu wa Baraza la Chuo Kikuu (2009 – 2013) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma (2013 hadi sasa).

Profesa Luoga aliyezaliwa mwaka 1958 ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alihitimu shahada ya kwanza ya Sheria UDSM
mwaka 1985.

Baadaye alikwenda kusoma Shahada ya Uzamili (LLM) katika chuo cha Queen’s University cha  Canada(1988).Mwaka 1988 alihitimu ya Uzamili ya Sheria za Kimataifa (MIL) katika Chuo cha Lund University cha Sweden (1991) naShahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Warwick cha Uingereza mwaka 2003.


MUGABE ‘ATUMBULIWA’ SIKU CHACHE BAADA YA KUTEULIWA BALOZI



Rais Robert Mugabe.



Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ametengua uteuzi wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye aliteuliwa kuwa
Balozi mwema wa Shirika hilo siku chache zilizopita.

Imedaiwa kuwa sababu za kutengua uteuzi huo ni kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa watu.
Tangu taarifa za uteuzi wake zisambae, viongozi wengi kutoka pande mbalimbali duniani walionekana kutokukubaliana na uteuzi
huo hivyo kukosoa uamuzi wa shirika hilo.

Mugabe ambaye ni mmoja wa marais waliokaa madarakani kwa muda mrefu barani Afrika amekuwa akishutumiwa kwa kukandamiza demokrasia nchini Zimbabwe ikiwa ni pamoja na kufanya mbinu ili kuweza kusalia madarakani hadi pale
atakapochoka mwenyewe.

Monday, 23 October 2017

Arsenal yainyoa bila maji Everton 5-2

Mesut OzilMesut Ozil alifunga bao la kwanza la Arsenal
Everton ilishuka katika ligi kuu baada ya kutandikwa mabao 5-2 na Arsenal katika uga wa Goodison Park.

Nacho Monreal, Mesut Ozil, Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey waliifungua Arsenal huku naye Wayne Rooney aliwafungia Everton bao lao la kwanza.

Oumar Niasse alifungua Everton bao la pili kabla ya Alexis Sanchez kuiongezea Arsenal bao la tano.

Wayne Rooney
Rooney aliifungia Everton bao la kwanza

Idrissa Gueye alitimuliia uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi ya njano mara mbili wakati Everton walikuwa chini kwa mabao 2-1.

Ushindi huo wa Arsenal ugenini uliipandisha ngazi juu ya Watford hadi nafasi ya tano katika jedwali huku Everton wakiwa hawajashinda katika mechi tano.

Sanchez
Sanchez aliongezea Arsenal bao la tano

Rais wa Somalia aizuru Uganda

Rais Farmaajo

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo yuko nchini Uganda kwa ziara rasmi .
Haijajulikana lengo la safari yenyewe lakini huenda inauhusiano na usalama wa mji mkuu wa nchi hiyo wa Mogadishu unaozidi kuzorota huku Uganda ikiwa na askari wengi kama walinda amani.
Ziara hii inafanyika wiki moja tu baada ya kutokea shambulio kubwa la kigaida nchini Somalia ambalo limesababisha vifo vya mamia ya watu.

Shambulio hilo ndilo baya sana kuwahi kutokea mjini Mogadishu kwani takriban watu 358 wanaripotiwa kuaawa na wengine kujeruhiwa huku 56 hawajulikani waliko.

Rais Museveni
Rais Museveni wa Uganda

Ingawa haijulikani lengo la safari hiyo, lakini wachambuzi wanahisi ziara hii inaweza kuwa ni moja wapo ya jitihada za Somalia kuomba usaidizi zaidi wa kijeshi kutoka Uganda hasa ikizingatiwa kwamba, Uganda ni miongoni mwa nchi zinazochangia wanajeshi wake Somalia.

Hata hivyo, swali ni je, iwapo wataongezewa nguvu inaweza kuleta tofauti yoyote? kwa sababu hivi sasa tayari Uganda ina idadi kubwa zaidi ya wanajeshi Somalia.

Uganda inachukuliwa kama mshirika wa karibu na Somalia na kuafuatia shambulio hilo rais Museveni alililaani vikali.

Hakusema ni hatua gani Museveni angefanya kuweza kuzua shambulio kama hilo lakini Uganda ina vikosi zaidi nchini Somalia vikiwa chini ya kivuli cha vikosi vya kulinda amani vya Muungano wa Afrika.

Uganda inachukuliwa kama mshirika wa karibu na Somalia na kuafuatia shambulio hilo rais Museveni alililaani vikali.

Hakusema ni hatua gani Museveni angefanya kuweza kuzua shambulio kama hilo lakini Uganda ina vikosi zaidi nchini Somalia vikiwa chini ya kivuli cha vikosi vya kulinda amani vya Muungano wa Afrika.

WAZIRI WA MAGUFULI ATANGAZA BOMOABOMOA KUBWA NCHI NZIMA




Bomoa bomoa kufanyika nchi nzima.



Hatimaye baada ya Bomoa bomoa kutikisa Mbezi ya Kimara,Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alpoenda kutatua mgogoro wa ardhi.
Waziri Lukuvi amesema tatizo la ujenzi holela linaanza pale ambapo Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzina Maafisa Mipangomiji wanaacha majengo yanaibuka katika miji yao bila kujua ujenzi huo una kibali au unajengwa katika kiwanja chenye hati na muhusika wa hati hiyo ndio anayejenga.

“Hatuwezi kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyonaagiza Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka x katika majengo yote yanayojengwa bilavibali na ujenzi unaofanywa kwenye viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.

Watu watakaokumbwa na bomoa bomoa hiyo ni wale waliojenga bila vibali, kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa pamoja nawaliojenga baada ya kuvamia maeneo.

Saturday, 21 October 2017

Kenyatta aonya wanaotishia kuvuruga uchaguzi Kenya

Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewatahadharisha wanaotishia maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo pamoja na maandalizi ya uchaguzi mpya kwamba watakabiliwa vikali.
Aidha, ametoa wito kwa wapiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi ambao umekumbwa na utata Alhamisi wiki ijayo 26 Oktoba.
Rais huyo amesema maafisa wa usalama wa kutosha wametumwa maeneo mbalimbali kuhakikisha kuna usalama siku hiyo.
"Tunapojiandaa kwa uchaguzi wa urais tareje 26 Oktoba, ni muhimu kudumisha amani, sawa na tulivyofanya (Agosti) na nyakati nyingine awali," amesema.
"Kupiga kura kuwachagua viongozi tunaowataka ni haki ambayo ilipiganiwa na mababu zetu, na lazima tuilinde."
"Sheria itatumika kwa njia sawa bila kujali hadhi yako katika jamii au siasa, hakuna atakayesazwa. Kwa wale wanaofana wakati wa vurugu, siku zenu zinafikia ukingoni, sheria itachukua mkondo wake na mtaadhibiwa ipasavyo."
Kiongozi huyo alikuwa akihutubu wakati wa sherehe ya Siku ya Mashujaa ambayo huadhimishwa kila tarehe 20 Oktoba kuwakumbuka mashujaa waliopigania uhuru pamoja na Wakenya wengine waliotoa mchango wa kipekee kwa taifa baada ya uhuru.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi huo wa Alhamisi na amesisitiza kwamba hakutakuwa na uchaguzi siku hiyo.
Badala yake amewahimiza wafuasi wake kuandaa maandamano kote nchini humo.
Kiongozi huyo wa upinzani ameongoza mkutano wa kisiasa eneo la Bondo, magharibi mwa Kenya ambapo amewahimiza Wakenya kuwa na umoja na kudumisha amani.
Bw Odinga amekuwa akishinikiza mageuzi yafanywe katika tume ya uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya.
Miongoni mwa mabadiliko hayo, alitaka afisa mkuu mtendaji Ezra Chiloba ang'atuke pamoja na maafisa wengine wakuu katika tume hiyo.
Taarifa zinasema Bw Chiloba ameamua kwenda likizo ya wiki tatu kuanzia Jumatatu, jambo ambalo litahakikisha kwamba hatakuwepo wakati wa kufanyika kwa uchaguzi.
UsalamaUsalama uliimarishwa uwanjani Uhuru Park wakati wa maadhimisho hayo
Mmoja wa waliohudhuria maadhimisho ya Mashujaa DeiMmoja wa waliohudhuria maadhimisho ya Mashujaa Dei

ZITTO AIBUA MAPYA BAADA YA ACACIA KUDAI HAINA HELA YA KULIPA






Wakati Watanzania wakiwa katika hali ya sintofahamu baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Acacia kudai kwamba haina pesa za kuilipa serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa juzi na Kampuni ya Barrick Gold Mining, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACTWazalendo),Zitto Kabwe ameibuka tena na kusema kwamba Serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Mhe. Kabwe amesema kuwa alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwaKampuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo (akiiita kishika uchumba) ambapo hata mwaka 2016 walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi waliahidi hivyo.

Amesema kwamba tangu juzi alishangaa sana kusikia serikali ikisema kwamba “Tumefanikiwa” kwani haikuwa ikizungumza nakampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni Barrick na kutokana na sheria ya makampuni, mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

“Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo jana. Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadikama waliyokuwa wameitoa jana na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Acacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo,” amesema Zitto.

Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa Dola milioni 300 (sawa na zaidi ya bilioni 660) kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro uliokuwepo awali.

Wednesday, 18 October 2017

Uchaguzi 2017: Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya Roselyn Akombe IEBC ajiuzulu

Roselyn Akombe 6 Julai 201

Roselyn Akombe

Mmoja wa maafisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi mpya wa urais kufanyika nchini humo.
Ametangaza kwamba anahofia usalama wake na hatarajii kurejea Kenya hivi karibuni.
Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.
Tume ya IEBC imesema imesikitishwa na hatua ya Dkt Akombe kujiuzulu na kuahidi kutoa taarifa ya kina baadaye. Mwenyekiti Wafula Chebukati anatarajiwa kuhutubia wanahabari baadaye leo.

 "Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati maisha ya watu yamo hatarini," amesema kwenye taarifa hiyo."Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani."
"Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.

Akombe

"Imekuwa vigumu kutokea kwenye televisheni kutetea misimamo ambayo natofautiana nayo kwa sababu ya kuwajibika kwa pamoja.

"Nimefikia uamuzi kwamba siwezi tena kutoa mchango wa maana kwa Tume na kwa taifa langu kama Kamishna."

Dkt Akombe alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la maafisa waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura.

Dkt Akombe alizuru Nyanza na maeneo ya Magharibi, ambayo ni ngome ya upinzani, wiki iliopita huku tume hiyo ikijaribu kuwafunza maafisa watakaosimamia uchaguzi huo.

Roselyn Akombe: Nahofia maisha yangu sirudi Kenya karibuni

Wakuu wa IEBC

Mwenyekiti: Wafula Chebukati

Naibu Mwenyekiti: Consolata Nkatha Maina

Makamishna:

Boya Molu

Paul Kibiwott Kurgat

Abdi Guliye

Margaret Wanjala Mwachanya

Afisa Mkuu Mtendaji/Katibu: Ezra Chiloba

Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, akiwa mbele ya mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa upinzani Nasa kwa zaidi ya kura 1.4 milioni.

Bw Odinga alipinga matokeo hayo mahakamani na Mahakama Kuu ikaamua ulijaa kasoro nyingi na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku sitini.

Tume ya uchaguzi ilitangaza tarehe mpya ya uchaguzi kuwa 26 Oktoba lakini Bw Odinga alijiondoa wiki iliyopita akisema mageuzi ambayo yalifaa kutekelezwa kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki hayajatekelezwa.

clouds stream