Wednesday 4 January 2017

Jeshi lamuunga mkono rais Jammeh nchini Gambia

Jenerali Badjie amuunga mko rais Jammeh licha ya mataifa ya magahribi kutoa vitisho vya kijeshi dhidi yake

Jenerali Badjie amuunga mko rais Jammeh licha ya mataifa ya magahribi kutoa vitisho vya kijeshi dhidi yake
img-20161130-wa0008

Mkuu wa jeshi la taifa la Gambia amemuunga mkono rais wa taifa hilo Yahya jammeh licha ya mgogoro unaondelea nchini humo.

Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais na Adama Barrow.

Awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo lakini akabadili nia siku kadhaa baadaye akitaja kuwepo kwa udanganyifu wa kura.

Katika barua kwa magazeti yanayounga mkono serikali, Jenerali Ousman Badjie aliahidi kwamba jeshi litamtii rais huyo.

Uingiliaji wa kati wa Jenerali Badjie unafuatia vitisho vya kijeshi vya jamii ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi ECOWAS iwapo Jammeh atakataa kuondoka madarakani ifikiapo Januari 19.

Rais Jammeh amesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itasababisha vita.Adama Barrow na rais Jammeh kulia
Adama Barrow na rais Jammeh kulia

Kundi la bwana Barrow awali lilikuwa limedai kuungwa mkono na Jenerali Badjie.

Hatua hiyo ya Jeshi inaonekana kuleta utata katika kuanzisha serikai mpya baada ya Jammeh iliokuwa madarakani kwa miaka 22.

Taifa hilo dogo la Afrika magharibi halijawahi kuwa na ukabidhi wa mamlka kutoka uongozi mmoja hadi mwengine kwa njia ya amani tangu taifa hilo lijipatie Uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1965.

Mzozo kuhusiana na matokeo ya uchaguzi umesababisha wasiwasi, huku mataifa jirani na jamii ya kimataifa yakimtaka rais Jammeh kuondoka mamlakani.

clouds stream