Wednesday 2 August 2017

Marekani yasema haina uadui na Korea Kaskazini

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amesema kuwa Marekani sio adui wa Korea Kaskazini

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson amesema kuwa Marekani sio adui wa Korea Kaskazini
IMG-20170426-WA0006

Serikali ya Marekani haitaki mabadiliko ya utawala Katika Korea Kaskazini, waziri wa mambo ya nje wa Marekani anasema, huku hofu ikitanda juu ya mpango wa silaha wa Pyongyang.

"Sisi si maadui zenu, " Rex Tillerson alisema, na kuongeza kuwa Marekani ilitaka mazungumzo wakati mmoja.

Wakati huo huo seneta wa chama cha Republican alisema rais Trump alihisi kuanza vita na Korea kaskazini ni chaguo

Pyongyang inadai kuwa jaribio lake la hivi karibuni la makombora linaweza kushambulia magharibi mwa Marekani na zaidi.

" Hatutaki mabadiliko ya utawala, hatulengi kuuangusha utawala, hatutaki kuharakisha muungano wa eneo la Peninsula, hatutaki sababu ya kutuma wanajeshi wetu kwenye eneo lenu ," alisema Bwana Tillerson, akimaanisha mpaka baina ya Korea kaskazini na Korea kusini.

"Sisi si maadui zenu, sisi si tisho kwenu , lakini munatuwekea tisho lisilo kubalikana lazima tujibu."

Jaribio la pili la kombora la masafa marefu linaloweza kshambulia bara jingine (ICBM) siku ya Ijumaa, lililosherehekewa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, lilikuwa ni jaribio la hivi karibuni kutekelezwa linalokiuka marufuku ya Umoja wa Mataifa

Rais Kim Jong un alisema kombora la masafa marefu linaweza kushambulia eneo lolote la Marekani
Rais Kim Jong un alisema kombora la masafa marefu linaweza kushambulia eneo lolote la Marekani

Majaribio ya hivi karibuni ya makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini yamesababisha hofu kubwa juu ya tishio la serikali ya Pyongyang dhidi ya Marekani , na kuzingatiwa kwa haja ya kuzuwia shambulio lolote nchini Marekani.

Hilo ndilo alilokuwa nalo akilini rais Trump katika mazungumzo juu ya vita na seneta Lindsey Graham.

Makao makuu ya wizara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon, yametoa taarifa za hivi karibuni juu ya hatua za kijeshi , lakini wakati huo huo wachambuzi wanasema kukabiliana na Korea Kusini itakuwa ni maafa.

Hilo limemfanya , Bwana Tillerson arudie kwa marefu kwamba Marekani haitaki mabadiliko ya utawala na kuongeza kuwa lengo ni kufanya mazungumzo, lakini ambayo hayana msingi kwamba Korea Kaskazini inaweza kuendelea kutunza silaha zake za nuklia

Serikali ya Pyongyang hata hivyo imekataa kata kata masharti ya aina hiyo.

clouds stream