Monday 10 July 2017

KAULI Ya SERIKALI KUHUSU RUFAA Ya UHAKIKI VYETI Kwa WALIMU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.

IMG-20170426-WA0006

Watumishi wa umma waliowasilisha vyeti vyao vya kuhitimu kidato cha nne, cha sita na ualimu kwa ajili ya rufaa katika Baraza la Mitihani la Taifa (NETA) kuhusu zoezi la uhakiki, wanatakiwa kuwasiliana na waajiri wao ili kupewa matokeo ya hatma ya rufaa kuhusu uhalali wa vyeti vyao.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Rais-Utumishi Kitengo cha Mawasiliano Serikali imebainisha kuwa ipo taarifa inayosambaa katika mitandao mbalimbali ikiwa ni majina ya wanaodaiwa kuwa watumishi wa umma na maeneo yao ya kazi ikiwa na kinachodaiwa matokeo ya rufaa zilizokatwa kuhusu uhalali wa vyeti vya elimu kwa wahusika.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Wananchi na watumishi wote wanaelezwa kuwa, serikali inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa na mawasiliano hivyo taarifa inayosambazwa haijatolewa na serikali na ipuuzwe.

clouds stream