Saturday 7 January 2017

Rais mpya wa Ghana kuapishwa leo

Bwana Akufo aliwania pia urais mwaka 2008 na 2012

Bwana Akufo aliwania pia urais mwaka 2008 na 2012
img-20161130-wa0008

Rais mpya wa Ghana ataapishwa hii leo, katika taifa ambalo limetajwa na wengine kama lenye kiwango bora zaidi cha Demokrasia Barani Afrika.

Nana Akufo-Addo, aliyekuwa wakati mmoja wakili wa haki za kibinadamu, alimshinda kiongozi wa sasa, John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Karibu viongozi 11 wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo, ambako hali ya usalama tayari imeimarishwa.

Baada ya kuapishwa kwake, viongozi wa Afrika watajadiliana jinsi ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia Yahya Jamme anakubali kuwa alishindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

clouds stream