Trump amekosolewa vikali kwa sera hiyo

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea marufuku yake ya muda ya kusafiri kwa watu wanaotoka katika nchi saba ambazo ni za kiislamu baada ya watu kuukosoa uamuzi huo huku wengine wakiandamana.
Katika taarifa ya maandishi, bwana Trump amevilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha taarifa kwamba marufuku hiyo ni kwa waislamu.
Amesema viza zitatolewa kwa wasafiri kutoka nchi zote ndani ya siku tisini.
Katika hali inayoonekana kulegeza msimamo wa amri ya kiutendaji iliyopitishwa siku ya Ijumaa, Reince Priebus, ambae ni kiongozi wa wafanyakazi wa serikali amesema marufuku hiyo haitawahusu wenye kuhodhi kadi za green, ambao wana haki ya kisheria kuishi nchini Marekani.
Mhariri wa BBC kaskazini mwa marekani amesema ikulu ya marekani imekosolewa vikali kwa sera hiyo.
