JK:Tanzania inaongoza kwa kuwa na vyombo vingi vya Habari

Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa
Ujerumani Joachim Gauck kwenye hotuba wakati akiongea na waandishi wa
Habari Ikulu jana.
Kauli hiyo ilitolewa na Rais wakati akijibu swali lililokuwa linahoji kwa nini Serikali imesitisha uingizaji wa gazeti la “The East African” wakati wa mkutano wake Rais Kikwete na Rais wa Ujerumani Joachim Gauck.
Pia aliongeza gazeti hilo alikufuata utaratibu na sheria na taratibu za nchi ndio maana Serikali imekutana na wahusika ili kuweza kuwaeleza nini cha kufanya.
Rais Kikwete aliyataja magazeti yanayomilikiwa na Serikali ambayo ni Daily News na Habari leo huku wagazeti ya watu binafsi ni mengi kama Nipashe,majira,Mwananchi,The Guardian,The Citizen na mengine mengi.