Wednesday 21 June 2017

Mghwira Abariki Shamba La Mbowe Kuharibiwa

Anna Mghwira Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Anna Mghwira  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
IMG-20170426-WA0006

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa dhidi ya shamba la Kilimanjaro Veggie linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, sio za kisiasa bali ni utaratibu wa kisheria wa kulinda vyanzo vya maji.

Mgwhira ametoa kauli hiyo alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali halisi ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomikiwa na Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai.

Amesema hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni sahihi katika kulinda vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu 81.

“Mmiliki wa shamba alikubali jambo hili na kukiri kuwa ni kosa kisheria na kukubali kuondoa mazao yake ifikapo Mei 23 baada ya kukubaliana na Mkuu wa Wilaya ya Hai ya kwamba atatumia miezi minne kuondoa mazao hayo lakini hakufanya hivyo,” amesema Mwenyekiti huyo wa zamani wa ACT­Wazalendo.

Awali akizungumzia hatua hiyo, Mbowe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuharibu miundombinu ya umwagiliaji katika shamba hilo la kisasa na kudai kitendo hicho kimemsababishia hasara ya mamilioni ya fedha na kukosesha ajira zaidi ya vijana 100.

Hatahivyo, amesema suala hilo linashughulikiwa na wanasheria wake na pindi litakapokamilika watachukua hatua.

clouds stream