Thursday 8 June 2017

ZITTO AFUNGUKA UTEUZI WA MGHWIRA , ATAKA WANACHAMA ACT WASILUMBANE NA ‘NYUMBU’

Image result for zitto kabwe
IMG-20170426-WA0006

Kiongozi wa Act­Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe hatimaye amefunguka na kuzungumzia kitendo cha Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Bi. Anna Elisha Mghwira kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Tayari chama hicho kimemuondoa mteule huyo mpya katika nafasi yake ya Uenyekiti na kupitia ukurasa wake wa facebook, Zitto Kabwe amefunguka yafuatayo;

Chama chetu cha Act Wazalendo ni kichanga Kwa umri lakini ni kibobevu kwenye Uongozi. Unajua uimara wa Vyama kwenye mitihani Kama Hii inayotukuta sisi. Tunavuka na Mola anatusaidia kuishinda mitihani.

Kuna ambao toka tuanzishe Chama wameshindwa kukubali hali halisi na ku move on. Kila siku wanatushambulia Kwa kejeli na maneno. Sisi hatuwajibu. Tunafanya yetu. Hatuwashangai maana tunawaongoza kwenye hoja. Tutaendelea kuwaongozakwenye hoja. Hatubabaishwi na kelele zao.

Hakuna Chama Cha Siasa nchi Hii kinaweza kuthubutu kubeza uwezo wetu wa hoja na kuchambua hoja. Kelele hatuna. Matusi hatuna. Kebehi hatuna. Hoja hapa ni mtakuja.

Wanachama 400,032 wa ACT Wazalendo mliotapakaa nchini nzima msiingie kwenye malumbano na nyumbu. Nyumbu hawawazi. Wanafuata tu. Wajibu wetu ni kuwaongoza nyumbu wavuke salama mto mara. Asili ya kuanzishwa kwetu ni kuukataa unyumbu. Tuendelee kuukataa unyumbu Kwa kumrejea Nkrumah ” Forward Ever, Backward Never “.

      Sisi ni Gogo la Udi. Unavyolichoma ndio linavyonukia.

                        Utu. Uzalendo. Uwajibikaji.

clouds stream