Tuesday 6 June 2017

Misri, Saudi Arabia na Bahrain kufunga anga zake kwa ndege za Qatar

qatar

shirika la ndege la Qatar
IMG-20170426-WA0006

Misri inafunga anga zake kwa ndege za Qatar katika mzozo wa kidiplomasia unaozidi kukua huku Saudi Arabia na Bahrain nazo zikitarajiwa kuchukua hatua kama hiyo leo Jumanne.

Nchi kadha zimekata uhusiano na Qatar, baada ya kuishutumu kwa kuunga mkono ugaidi katika eneo la Ghuba.

Raia wa Qatar nchini Bahrain, Saudi Arabia na Muungano wa Milki ya nchi za kiarabu wamepewa muda wa wiki mbili kuondoka.

Qatar inakana kunga mkono wanamgambo na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni ametaka kuwepo mazungumzo.

Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo hautaathiri chochote katika utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharula tangu mzozo huo ulipoibuka siku ya Jumatatu wiki hii.

clouds stream