Tuesday 4 November 2014

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

JENGO LILILOSHAMBULIWA NA OSAMA BIN LADEN LAZINDULIWA

Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York
Kituo cha One World Trade Centre chapita majengo yote katika mtaa wa Manhattan, jijini New York.
Miaka 13 baada ya majengo ya awali ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa, WTO kuharibiwa katika shambulio la kigaidi likiongozwa na Osama Bin Laden la Septemba 11, 2001, kituo hicho kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara.
Jengo hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Jengo hilo lenye urefu wa mita 541 kwenda juu liko katikati ya eneo la New York, ikiwemo sehemu ya eneo la kumbukumbu la majengo ya zamani na makumbusho yaliyofunguliwa mwaka huu
Jengo hilo limekodishwa kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya Utawala wa Huduma imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi za mraba 275,000.
“Mwonekano wa angani wa jiji la New York umerejea tena,” anasema Patrick Foye, mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, ambayo yanamiliki eneo hilo lililorejeshewa hali yake.

clouds stream