Monday 10 November 2014

RAIS KIKWETE AFANYIWA UPASUAJI TEZI DUME

RAIS KIKWETE AFANYIWA UPASUAJI TEZI DUME


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Hospital ya
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Hospital ya Johns Hopkins nchini Marekani.
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja  na nusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete anaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

clouds stream