Rais wa Ujerumani awasili nchini Tanzania

Rais
wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Ghalib Billal
akiwa mwenye furaha tele mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mhe.
Joachim Gauck

Rais
wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akiwa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Ghalib Billal wakifurahia kwa pamoja
burudani kutoka kwa vikundi mbarimbali vya burudani.
Pia baada ya kumaliza mazungumzo wa Rais Kikwete atakutana na wafanyabiashara wa Dar es Salaam na uongozi wa kanisa la KKKT kabla ya kuelekea Zanzibar kukutana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kabla ya kuhitimisha ziara yake tarehe 6 atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti na pia makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki na Mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu huko Arusha.