Wednesday, 4 February 2015

Afisa Elimu avuliwa madaraka kwa ufisadi wilayani Mbinga


Afisa Elimu avuliwa madaraka kwa ufisadi wilayani Mbinga




Moja ya msingi wilayani Mbinga.
Moja ya msingi wilayani Mbinga.
Ruvuma, Afisa elimu msingi  wa wilaya ya Mbinga Bw. Daniel Mkali amevuliwa madaraka  kwa tuhuma za kubwa nne ambazo ni kusajili  asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyojulikana kwa jina la (UWEKAMBI) umoja wa waratibu elimu kata ya Mbinga na kuwaagiza walimu wakuu wa shule za msingi wilayani humo kuhamishia fedha zote za capitation na michango ya Umitashumta ambazo ni jumla ya shilingi milioni 232.
Aidha, katika fedha hizo shilingi milioni 60 ni michango ya Umitashumta, milioni 10 ni michango ya wazazi na shilingi milioni 61 ni fedha kwa ajili ya capitation na mitihani zilipelekwa kwenye akaunti yenye namba 61714000405 iliyopo katika benki ya NMB tawi la Mbinga.
Akizungumzia hatua hiyo  ya  kumvua wadhifa huo pamoja na kumshusha cheo na kutakiwa kupangiwa shule ya kufundisha mwenyekiti wa halmashauri  ya Mbinga Alanus  Ngahi, amesema tuhuma nyingine inayomkabili   ni kughushi nyaraka kwa lengo la kutoa fedha kupitia ununuzi wa mafuta ya diesel lita 5500 na petrol lita 5500.
Kuwaagiza walimu wakuu wachangie fedha za kupiga picha wanafunzi wa darasa la saba pamoja na fedha kwa ajili ya TSM 9 kwa maelekezo hayo ni kosa kwa sababu alikuwa akijua kuwa gharama za TSM 9 hugharamiwa na serikali kwa asilimia mia moja.
Tuhuma nyingine  ni kumdanganya mwajiri kuwa hakujakusanywa fedha yoyote kutoka kwa wazazi na hakuna fedha ya capitation iliyopelekwa kwenye akaunti hiyo ya UWEKAMBI. Kufuatia  hatua Afisa elimu huyo anatarajiwa kuchuliwa hatua  nyingine za kinidhamu.

clouds stream