Sunday 28 May 2017

KAGAME ATANGAZA KUACHIA MADARAKA RWANDA

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

IMG-20170426-WA0006

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa ukomo wa utawala wake utakuwa mwaka 2024 na kuwataka Raia wa Rwanda kuanza kuanza kufikiria mtu mwingine baada ya muda huo.

Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu nchini Rwanda unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu na kusema kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.

“Inawezekana natakiwa niliangazie suala hili katika siku chache zijazo nitakapoanza mbio za urais. Kuna aina ya makubaliano kati yangu mimi na RPF­Inkotanyi kwa upade mmoja, na raia wa Rwanda kwa upande mwingine,” amesema Kagame.

“Raia, kupitia kura ya maoni ya Disemba 2015, waliniomba niendelee kuwaongoza nikakubali, ila muda mwafaka wa kupumzika umewadia na waomba waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba,” ameongeza Kagame kwenye mahojiano yake na mtandao wa Jean Afrique.

Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.

Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe katiba ili Kagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.

Bunge lilifanya hivyo ili limruhusu rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania awamu zingine mbili hadi mwaka 2024.

clouds stream