Sunday 14 May 2017

Microsoft: Shambulizi la Kompyuta liwe funzo

Shambulizi la mitandaoni laathiri mataifa 150

Shambulizi la mitandaoni laathiri mataifa 150

Shambulizi la uhalifu wa mitandaoni lililoathiri mataifa 150 tangu siku ya Ijumaa linafaa kuchukuliwa kama funzo, Microsoft imesema.

Kampuni hiyo ya kompyuta inasema kuwa hatua ya serikali hizo kutoimarisha programu zao mara kwa mara ndio sababu ya tatizo hilo.

Kirusi hicho kilichukua fursa ya dosari ya toleo la programu ya Microsoft Windows lililogunduliwa na majasusi wa Marekani.

Kuna hofu ya shambulio jingine la kirusi hicho cha 'ransomware' huku raia wakitarajiwa kurudi kazini siku ya Jumatatu.

Kampuni nyingi zimeajiri wataalam waliofanya kazi wikendi kuzuia maambukizi mapya.

Kirusi hicho kiliteka faili na kutaka kulipwa dola 300 kama kikombozi.

Kusambaa kwa kirusi hicho kulipungua wikendi lakini huenda hali hiyo ikawa ya muda ,wataalam wameonya.

Zaidi ya Komyuta 200,000 zimeathiriwa kufikia sasa.

Taarifa kutoka kwa rais wa Microsoft na afisa mkuu wa maswala ya sheria Brad Smith siku ya Jumapili ilikosoa vile serikali zinavyoweka taarifa zao kuhusu dosari za kiusalama katika mifumo ya kompyuta.

''Tumeona dosari zinazohifadhiwa na CIA zinaonekana katika Wikileaks na sasa dosari ilioibwa kutoka kwa NSA imeathiri wateja kote duniani'', aliandika

''Ukilinganisha na silaha za kisasa hiyo inamaanisha kwamba Silaha za Marekani kama vile Tomahawk zingekuwa zimeibwa''.

clouds stream