HOUSE FOR SALE: Located at Ununio, 7 bed rooms, 2 sitting rooms,
kitchen, store and a libraly. It has a car parking, it has a dept to
I&M Bank. PRICE is TSH.250 mil negotiable.
Thursday, 26 February 2015
Arsenal yashindwa kutamba nyumbani, yakubali kipigo cha 3-1
Arsenal yashindwa kutamba nyumbani, yakubali kipigo cha 3-1
Matumain ya Arsenal yapo mashakani kwenye michuano ya ligi ya mabigwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa Monaco kwenye mechi ya kwanza hatua ya 16 bora mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates.
Geoffrey Kondogbia alliifungia Monaco goli la kuongoza kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Tottenham kuongeza goli la pili kipindi cha pili wakati Arsenal wao walishindwa kutumia vyema nafasi zao walizopta.
Olivier Giroud na Danny Welbeck walikosa magoli ili kuirejesha Arsenal kwenye mchezo kabla ya Alex Oxlade –Chamberlain kuifungia timu yake dakika za majeruhi, lakini Ferreira Carrasco akafunga goli la tatu kwa Monaco kwenye dakika za nyongeza za mchezo huo.
Arsenal waliunza vizuri mchezo kwa kumiliki mpira vizuri dakika za mapema za kipindi cha kwanza lakini walishindwa kutumia nafasi hiyo kupata goli, dakika chache baadae Monaco walianza kucheza mpira wa kasi na kuwafanya Arsenal kuwa kwenye wakati mgumu kwa muda mwingi wa mchezo.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa klabu ya Monaco kwenye uwanja wa Emirates ambao unawaweka vijana wa mzee Wenger kwenye mazingira magumu ya kufuzu kwa hatua inayofuata ya robo fainali, Arsenal kama watatolewa kwenye hatua hiyo itakua ni mara ya tano mfululizo kutoka kwenye hatua ya 16 bora.
Kwenye mchezo mwaingine uliopigwa huko Ujerumani, wenyeji timu ya Bayern Liverkusen wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Atletico Madrid huku goli pekee la washindi likifungwa na Calhanoglu.
Ligi kuu Ugiriki imesimamishwa kwa muda usio julikana
Ligi kuu Ugiriki imesimamishwa kwa muda usio julikana
Mechi za ligi kuu nchini Ugiriki zimeahirishwa kwa muda usiojulikana baada ya kutokea kwa vurugu kubwa.
Uamuzi huo umefikiwa na bodi ya ligi ‘Super ligi’ ya nchini Ugiriki baada ya kundi la mashabiki kuvamia uwanja kwenye mechi ya Athens ‘Derby’ mwishoni mwa wiki iliyopita, chama tawala cha Syriza kilicho chaguliwa hivi karibuni kimedhamiria kudhibiti matatizo ya vurugu zitokanazo na mashabiki.
“Tumearifiwa kwamba Super ligi imesimamishwa kwa muda usiojulikana,” raisi wa Supa ligi Giorgos Borovilos amewaambia waandishi wa habari.
“Tuna serikali mpya sasa ambayo inatarajia kulileta swala hili kwenye majadiliano na utekelezaji wa kisheria utafuata kulingana na tatizo,” aliongeza.
Waziri wa michezo wa Ugiriki Stavros Kontonis amekutana na Waziri Mkuu Alexis Tsipras siku ya Jumatano iliyopita ili kujadili swala hilo na watakutana na Rais wa Super ligi Giorgos Borovilos.
Borovilos amesema bado haijajulikana mechi hizo zitasimamishwa kwa muda gani na kwa masharti gani, na akaongeza kuwa hakuna chochote kilichofanyika kwa muda wa wiki moja au mbili sasa.
“Serikali inataka mechi ziendelee haraka iwezekanavyo, lakini wanataka kuona hatua zikichukuliwa kutoka kwetu sote,” alisema Borovilos.
“Kutakua na majadiliano kati yetu, bodi ya Hellenic Football Federation (EPO) pamoja na ligi ya mpira wa miguu ambapo tutaona ni kwa jinsi gani tutaunda muundo wa ulinzi na sheria ili kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu unakua salama,” alisisitiza.
Hii ni mara ya tatu msimu huu kwa soka la kulipwa nchini Ugiriki kusimamishwa kwa sababu za vurugu.
Mechi zilisitishwa kwa wiki moja mwezi Septemba mwaka jana kufuatia kifo cha shabiki wa soka baada ya vurugu kwenye ligi daraja tatu kati ya Ethnikos Piraeus dhidi ya Irodotos.
Mamlaka zilisitisha michezo mwezi Novemba mwaka jana baada ya Christoforos Zografos, mkurugenzi saidizi wa kamati ya marefa wa kati (KED), alipo chukuliwa na kukimbizwa hospitali kufuatia kujeruhiwa kutokana na vurugu zilizo zuka uwnjani.
Walemavu wa ngozi kuitikisa Ruvuma kwa maandamano
Walemavu wa ngozi kuitikisa Ruvuma kwa maandamano
Maandamano makubwa kupinga mauaji pamoja na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yanatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma machi 2 mwaka huu.
Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa Ruvuma, Amini Mapunda amesema kwamba lengo la maandamano hayo ni kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kubainika na tuhuma za kuhusika na mauaji ya albino kwa madai kwamba baadhi yao wamekamatwa lakini mwenendo wa kesi zao bado haueleweki.
Mauaji ya Albino pamoja na wazee nchini Tanzania yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina, utajiri ama nafasi mbalimbali za kisiasa kwa imani za kishirikina huku serikali ikishindwa kuchukua hatua kali kwa wahusika suala linalopelekea mauaji hayo kuendelea.
Kwa upande wake mwenyekiri wa shirika la ROA, Mathew Ngalimanayo amesema kuendelea kwa mauaji hayo inatokana na jamii kukosa hofu ya mungu na wakati mwingine familia husika zikihusika kutokana na hali ngumu ya maisha hivyo kushawishika kirahisi.
Chenge awasilisha utetezi Baraza la Maadili, hatma yake kujulikana kesho
Chenge awasilisha utetezi Baraza la Maadili, hatma yake kujulikana kesho
Aidha, Andrew Chenge miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ni ya ukiukwaji wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma na alipokuwa mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa Washauri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.
Ambapo ilielezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sheria.
Kufuatia tuhuma hizo , Chenge aliweza kujitetea kwa kuiwasilisha oda maalum ya utetezi wake dhidi ya madai anayodaiwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Maadili anayeshughulikia mashauri hayo Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema wataenda kukaa na kupitia oda hiyo ya Chenge na kisha watatoa maamuzi siku ya februari 26 mwaka huu ambayo ni kesho.
Katika hatua nyingine Baraza hilo la Maadili kesho litaendelea tena na shauri hilo la Chenge pamoja na viongozi wengine wa umma akiwemo aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.Anna Tibaijuka.
Urais 2015: CCM kutegua kitendawili cha makada sita waliofungiwa
Urais 2015: CCM kutegua kitendawili cha makada sita waliofungiwa
Chama cha Mpinduzi (CCM) kupitia kamati kuu ya chama cha mapinduzi (CC), kinarajia kutoa majibu ya makada sita waliofungiwa kutokana na kuanza kampeni za kugombea urais kabla ya muda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Itikadi na unezi CCM Nape Nnauye imesema kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinnduzi Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuongoza kikao kamati kuu ya Chama hicho Februari 28,2015 jijini Dar es salaam. Katika taarifa hiyo haijafafanua kama kuna ajenda zitakazo zungumzwa katika kikao hicho.
Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu kimoja kutoka ndani ya Chama hicho kimeaimbia Hivisasa kuwa katika kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM, Philip Mangula, atawasilisha ripoti yake ya tathmini dhidi ya makada sita kuona kama walitekeleza adhabu waliyopewa.
Makada ambao waliangukiwa na adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja ni pamoja na mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Makada hao walitakiwa kutojihusisha na harakati zozote zinazoashiria kampeni ya kushawishi kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.
Kutokana na kikao hicho inawezekana kuwa wapo watakaotangazwa kuwa huru. Hata hivyo kwa wale ambao bado walikuwa wakiendelea na harakati za kufanya kampeni ya kushawishi kinyume cha utaratibu wanaweza kupoteza sifa za kuwania urais mwaka huu.
Tuesday, 24 February 2015
Julio atua Coastal Union kutoa msaada
Julio atua Coastal Union kutoa msaada
Julio ambaye amefanikiwa kuipamdisha daraja Mwadui FC na pia kuipa ubingwa wa ligi daraja la kwanza ametua kwenye kikosi cha Coastal Union kwa ajili ya kushirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo Mkenya James Nandwa ili kusaidiana kwa kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michezo iliyobaki.
Julio amesema Coastal ni timu yake na akiwa hapo anajiona yupo nyumbani na amewaahidi mashabiki na wapenzi wa Coastal watarajie mambo mazuri kutoka kwake akishirikiana na kocha mkuu wa timu hiyo.
“Coastal ni timu yangu na wameniomba nije nitoe msaada, kuanzia sasa timu itatisha maana mgonjwa kapata daktari wapenzi na mashabiki wasubiri raha. Nimesha maliza kujenga daraja Mwadui nimekuja kupandisha ghorofa Coastal,” ametamba Julio.
Kwa siku za hivi karibuni, timu ya Coastal Union imekua na matokeo mabovu na ilipoteza mchezo wake wa mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Barcelona, Juventus zatamba ligi ya mabingwa Ulaya
Barcelona, Juventus zatamba ligi ya mabingwa Ulaya
Manchester City ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Etihad imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Barcelona katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Luis Suarez alifunga magoli yote mawili kwa upande wa Barcelona katika dakika ya 16 na 30 akipokea pasi za mwisho kutoka kwa Jord Alba wakati Sergio Aguero ameifunga City bao la kufutia machozi katika dakika ya 69 akimalizia pasi ya David Silva.
Dakika ya 74 mlinzi wa Manchester City, Gael Clichy alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano. Nyota wa Barcelona Lionel Messi amekosa penalti dakika ya 90 baada ya mlinda mlango Joe Hart kupangua mkwaju huo.
Katika mchezo mwingine uliopigwa Italia, Juventus imetumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Juventus Stadium kuwaadhibu Borrusia Dortmundkwa goli 2-1 katika mchezo wao wa kwanza.
Carlos Tevez aliifungia Juventus goli la kuongoza katika dakika ya 13, lakini Marco Reus alisawazisha dakika tano baadaye.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Alvaro Morata aliandika bao la pili lililoduma mpaka dakika 90 ya mchezo.
Timu hizo zitacheza mechi za marudiano majuma mawili yajayo ili kuamua nani atasonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.
Iringa: Wananchi wapigana na Polisi, kituo cha polisi chachomwa moto
Iringa: Wananchi wapigana na Polisi, kituo cha polisi chachomwa moto
Vurugu zimeibuka mkoani Iringa kati ya wananchi na askari wa jeshi la
Polisi katika kituo cha Polisi cha Ilula kufuatia mwanamke ambaye ni
mama ntilie kufariki dunia wakati akiwakimbia Polisi waliokuwa katika
msako maalumu dhidi ya wafanyabiashara hao.
Kwa mujibu wa mwananchi ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye mtandao wa Hivisasa amesema kwamba kifo cha mwanamke huyo kimetokea wakati wa Purukushani hizo ambapo alianguka na kufariki dunia hapo hapo wakati anawakimbia askari hao.
Aidha, inadaiwa kuwa kufuatia tukio hilo Wananchi walipandwa na hasira na kuamua kuvamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Iringa zinaendelea ili azungumzie tukio hilo.
Kwa mujibu wa mwananchi ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye mtandao wa Hivisasa amesema kwamba kifo cha mwanamke huyo kimetokea wakati wa Purukushani hizo ambapo alianguka na kufariki dunia hapo hapo wakati anawakimbia askari hao.
Aidha, inadaiwa kuwa kufuatia tukio hilo Wananchi walipandwa na hasira na kuamua kuvamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Iringa zinaendelea ili azungumzie tukio hilo.
Sunday, 22 February 2015
Sherehe ya kuzaliwa Mugabe kuzizima Zimbabwe
Sherehe ya kuzaliwa Mugabe kuzizima Zimbabwe
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anatarajia kuadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa aina ya kipekee. Mugabe anatimiza umri wa miaka 91 akiwa ni kiongozi mzee kabisa dunia ambapo amekuwa madarakani kwa miaka 36.
Anatarajiwa kufanya sherehe kubwa katika uwanja wa golf huko Victoria Falls, inakisiwa sherehe yenyewe itagharimu dola milioni moja. Sherehe hiyo itafanyika wiki ijayo.
Maelfu ya watu watahudhuria karamu hiyo, ambapo kutachinjwa ndovu, nyati, paa na simba mmoja. Shirika la habari la taifa linasema wananchi watalipia dhifa hiyo.
Mji wa Baga wakombolewa kutoka kwa Boko Haram
Mji wa Baga wakombolewa kutoka kwa Boko Haram
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeukomboa mji wa Baga, kaskazini mashariki mwa nchi ambako mamia ya watu waliuawa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram mwezi uliopita.
Jeshi lilisema kumetokea mapambano makali na wapiganaji hao Waislamu na hasara ilikuwa kubwa.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, lilisema kuwa watu kama 2,000 waliuwawa Boko Haram ilipoiteka Baga shambulio lao kubwa kabisa.
Serikali ya Nigeria ilisema watu 150 walifariki katika mji huo. Baga iko kando ya Ziwa Chad kwenye jimbo la Borno, Boko Haram waliposhambulia maelfu ya watu walivuka ziwa kutafuta hifadhi nchini Chad.
Mji wa Baga wakombolewa kutoka kwa Boko Haram
Mji wa Baga wakombolewa kutoka kwa Boko Haram
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeukomboa mji wa Baga, kaskazini mashariki mwa nchi ambako mamia ya watu waliuawa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram mwezi uliopita.
Jeshi lilisema kumetokea mapambano makali na wapiganaji hao Waislamu na hasara ilikuwa kubwa.
Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, lilisema kuwa watu kama 2,000 waliuwawa Boko Haram ilipoiteka Baga shambulio lao kubwa kabisa.
Serikali ya Nigeria ilisema watu 150 walifariki katika mji huo. Baga iko kando ya Ziwa Chad kwenye jimbo la Borno, Boko Haram waliposhambulia maelfu ya watu walivuka ziwa kutafuta hifadhi nchini Chad.
HOUSES FOR SALE
HOUSE FOR SALE: A house located at Mbezi Luxury is there for sale, it has three bed rooms, it is wihin a large plot. PRICCE is TSH. 25mil.
Thursday, 19 February 2015
Baloteli aendeleza vituko Liverpool
Baloteli aendeleza vituko Liverpool
Gerard alikasirishwa kwa kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kwa Baloteli kupiga penati ya dakika ya 85 huku anajulikana mpigaji wa penati hiyo ni Jordan Henderson kwenye mchezo wa kombe la Uropa dhidi ya timu ya Besiktas ya Uturuki.
Balotelli alifunga penalti hiyo na kuiwezesha Liverpool kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya Uropa unaozishirikisha timu 32 uliochezwa Alhamisi katika uwanja wa Anfield.
Balotelli ana rekodi nzuri kwenye upigaji wa penati katika penati 29 za klabu na timu ya taifa alizopiga amefunga penati 27.
Gerrard amesema: “Henderson ni nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali hiyo.”
Gerrard ambaye kwa sasa ni majeruhi, alikuwa mchambuzi katika matangazo ya mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya nchini Uingereza.
Pia Gerard alimsifu kwa kufunga penati hiyo hila si jambo zuri wachezaji kuzozana wakati mpigaji wa penati anajulikana, Kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers akuzungumza jambo lolote kuhusu jambo hilo.
Southampton wasajili mchezaji wa Uganda
Southampton wasajili mchezaji wa Uganda
Baada ya kusajili mchezaji kutoka Kenya Victor Wanyama sasa timu hiyo ya ligi kuu ya Southampton nchini Uingereza imeamia nchini Uganda na sasa ni kijana wa miaka 19, Bevis Kristofer Kizito Mugabi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Mlinzi huyo licha ya wazazi wake wote wawili kuwa ni waganda bado ana uraia wa nchi mbili ambazo zinampa nafasi ya kuchezea timu ya taifa ya Uganda kwakuwa bado hajachezea timu ya wakubwa ya Uingereza.
Akiongea kwenye mtandao wa timu amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo baada ya timu ya awali ya Fulham kumuacha kwenye msimu wa 2011.
“Nimefurahi kupata nafasi hii, nimesaini na kila kitu kimekamilika. Lengo langu ni kucheza katika kikosi cha kwanza. Nitafanya kazi kwa bidii mazoezini na wakati wa mechi,” amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 19.
Mauaji ya Albino Geita Baba mzazi awekwa Lupango
Mauaji ya Albino Geita Baba mzazi awekwa Lupango
Jeshi la Polisi mkonai Geita Polisi linamshikilia baba mzazi wa mtoto aliyeuawa anayefahamika kama Bahati Misalaba mkazi wa kitongoji cha Mapinduzi katika kijiji cha Lumasa, wilayani Chato, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo amesema mtoto Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi (albino), aliyetekwa katika Kijiji cha Ilelema wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, mwili wake umekutwa ukiwa umefukiwa huku umenyofolewa miguu na mikono.
Ameongeza kuwa katika tukio hilo, watekaji waliokuwa na silaha mbalimbali za jadi, walimjeruhi pia Ester Bahati (30), ambaye ni mama wa mtoto ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Ametoa mwito kwa wananchi kutoruhusu tukio lingine la namna hiyo litokee, badala yake wachukue hatua mapema kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola viweze kudhibitiwa.
Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti Jumuiya ya Afrika Mashariki
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria. Katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Desemba mwaka jana, lakini hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini Marekani
Marais wote watano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa hayo, kujadiliwa katika kikaohicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kuomba uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa.
Magaidi wengine 4 watiwa mbaroni Tanga
Magaidi wengine 4 watiwa mbaroni Tanga
Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na viongozi wa jeshi la polisI jijini Tanga wamesema kwamba baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa ni wenye asili tofauti wakiwemo wenye asili ya kiarabu huku wengine wakiwa na asili ya kisomali ambao wote kwa pamoja wamekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Nao wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wakielezea jinsi walivyowadhibiti watuhumiwa ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa wamechoka katika vichaka vilivyopo pembeni mwa mapango ya maji moto yaliyokuwa yakihifadhi wahalifu yaliyopo kilomita 5 kutoka katika yale mapango ya amboni.
Inadiwa kuwa kukaa na njaa ndio sababu kuu iliyowafanya kuwakamata kiurahisi kisha kuwapigia simu askari wa jeshi la wananchi kwa lengo la kuwakabidhi watuhumiwa.
Kituo cha Polisi Vingunguti chazinduliwa leo
Kituo cha Polisi Vingunguti chazinduliwa leo
Aidha, Kituo hicho kimezinduliwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova. Hatua inafuatia eneo la vingunguti kutokuwa na kituo cha polisi kwa muda mrefu suala lilipelelekea kukithiri kwa vitendo uhalifu.
Nao wananchi wamelipongeza jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa kujenga kituo hicho suala ambalo litapelekea kudhibiti uhalifu pamoja na kuimarisha ulinzi wa mali za wa wananchi.
Watu wawili wafariki wakijaribu kuiba petroli
Watu wawili wafariki wakijaribu kuiba petroli
Taarifa za polisi zinasema watu hao ni Maria Pajela, 18, na William Paschal, 38 na wakazi wengine kwenye kijiji hicho waliiba mafuta kwenye kwenye gari lililokuwa limebeba kiasi cha lita 41,000.
Dereva wa gari hilo Zawadi Nyato, 46, na konda wake Bw.Frank Yohana, 24, wote ni wakazi wa Mbeya na wliokolewa na wasamalia na kupelekwa hospitali kupata huduma.
Taarifa zinasema baada ya gari hilo kuanguka wanakijiji walivamia na kuanza kuiba mafuta, majeruhi 18 wamepelekwa kwenye hospitali ya Igongwe.
Rais Kikwete ateua wakuu wa Wilaya wapya 27
Rais Kikwete ateua wakuu wa Wilaya wapya 27
\
RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA
27, Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42
kwenye vituo vyao vya zamani.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko
ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya
kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya
zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na
kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana na wakuu wa wilaya watatu
kufariki dunia; kupandishwa cheo wakuu wa wilaya watano, kupangiwa
majukumu mengine wakuu wa wilaya saba na kutenguliwa kwa uteuzi wa wakuu
wa wilaya 12.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema, Rais
Kikwete amewabadilisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 64 na kuwabakiza
kwenye vituo vyao vya zamani wakuu wa wilaya 42
Wakuu wa Wilaya wapya 27 walioteuliwa ni
Mariam Ramadhani Mtima anayeenda Ruangwa; Dk. Jasmine B. Tiisike
anayeenda Mpwapwa; Pololeti Mgema (Nachingwea); Fadhili Nkurlu anayeenda
Misenyi; Felix Jackson Lyaniva anayeenda Rorya na Fredrick Wilfred
Mwakalebela anayeenda wilaya ya Wanging
Wengine na vituo vyao kwenye mabano ni
Zainab Rajab Mbussi (Rungwe); Francis K. Mwonga (Bahi); Kanali
Kimiang;ombe Samwel Nzoka (Kiteto), Husna Rajab Msangi (Handeni),
Emmanuel J. Uhaula (Tandahimba); Mboni Mhita (Mufindi); Hashim S.
Mgandilwa (Ngorongoro); Mariam M. Juma (Lushoto); Thea Medard Ntara
(Kyela); Ahmad H. Nammohe (Mbozi); Shaban Kissu (Kondoa) na Stephen
Zelothe (Musoma)
Wengine ni Pili Moshi (Kwimba); Mahmoud
A. Kambona (Simanjiro); Glorius B. Luoga (Tarime); Zainab R. Telack
(Sengerema); Bernard Nduta (Masasi); Zuhura Mustafa Ally (Uyui); Paulo
Makonda (Kinondoni); Mwajuma Nyiruka (Misungwi) na na Maftah Ally
Mohamed (Serengeti)
Wakuu wa Wilaya saba ambao uteuzi wao
umetenguliwa lakini watapangiwa kazi nyingine ni Brig. Jenerali Cosmas
Kayombo aliyekuwa Simanjiro; Kanali Ngemela E. Lubinga (aliyekuwa
Mlele); Juma S. Madaha (aliyekuwa Ludewa); Mercy E. Silla (aliyekuwa
Mkuranga); Ahmed R. Kipozi (aliyekuwa Bagamoyo); Mrisho Gambo (aliyekuwa
Korogwe) na Elinas A. Pallangyo (aliyekuwa Rombo).
Waziri Mkuu pia aliwataja Wakuu wa
Wilaya 12 ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na sababu za umri,
kiafya na kuimarisha utendaji Serikaini na wilaya zao kwenye mabano kuwa
ni James K. Ole Millya (Longido); Elias Wawa Lali (Ngorongoro); Alfred
Ernest Msovella (Kongwa); Danhi Beatus Makanga (Kasulu); Fatma Losindilo
Kimario (Kisarawe); Elibariki E. Kingu (Igunga); Dk. Leticia Moses
Warioba (Iringa); Evarista N. Kalalu (Mufindi); Abihudi M. Saideya
(Momba); Martha J. Umbulla (Kiteto); Khalid J. Mandia (Babati) na Elias
Goroi (Rorya)
Boko Haram 300 wauawa Nigeria ?
Boko Haram 300 wauawa Nigeria ?
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua zaidi ya wapiganaji 300 wa
Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kukomboa tena miji kadhaa
iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.
Mwili wa Mtoto Mwenye ualbino wapatikana msituni
Mwili wa Mtoto Mwenye ualbino wapatikana msituni
Mwili wa mtoto wa mwaka mmoja mwenye ulemavu wa ngozi Yohana Bahati aliyeporwa mikononi mwa mama yake juzi Mkoani Geita, umeonekana jana jioni ukiwa umekatwa miguu na mikono yote na kufukiwa ardhini kwenye hifadhi ya msitu wa Biharamulo, Wilayani Chato.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema mwili wa mtoto huyo umebainika jana majira ya saa 12:30 jioni ukiwa umefukiwa kwenye eneo ambalo linashamba la mahindi.
Mtoto mwingine mwenye ulemavu wa ngozi aliyeporwa mwezi desemba mwaka jana bado hajapatikana hadi leo licha ya jeshi la Polisi kungatangaza kutoa zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazo saidia kupatikana mtoto huyo.
Mauaji, ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi bado ni changamoto licha ya serikali kutafuta mbinu za aina mbalimbali kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo kuwapiga marufuku wapiga ramli.
Wednesday, 18 February 2015
Urais 2015: Makaidi ajitosa UKAWA
Urais 2015: Makaidi ajitosa UKAWA
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi amesema tayari chama chake kimeshapendekeza jina lake kuwa miongoni mwa vigogo watakaoshindanishwa kwenye kinyang’anyiro hicho ili lipatikane jina moja litakaloiwakilisha UKAWA kupambana na chama tawala cha Mapinduzi.
Aidha, makubaliano ya umoja huo yanaelekeza vyama kupendekeza jina moja litakalowakilishwa katika Kamati ya Wataalamu ya Ukawa kabla ya kushindanishwa na majina mengine.
Kwa upande wa Vyama vya NCCR Mageuzi na Chadema bado havijaonyesha mwelekeo wa kupatikana jina la mgombea wa urais kutokana na michakato inayoendelea ndani ya vyama hivyo.
Uhuru kenyatta azindua kampeni mpya ya kondomu kwa vijana
Uhuru kenyatta azindua kampeni mpya ya kondomu kwa vijana
Sera ya uhamiaji ya Rais Obama bado kitendawili
Sera ya uhamiaji ya Rais Obama bado kitendawili
Akizungumza Ikulu ya nchi hiyo, Bwna Obama amesema sheria hiyo na historia viko upande wa utawala wake.
Wizara ya Usalama wa Ndani ya nchi imesema itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama na kwamba utawala umechukua mwelekeo mzuri kwa mujibu wa utawala wake wa sheria, lakini imeeleza kuwa kwa sasa itabidi ikubaliane na uamuzi wa mahakama.
Mageuzi ya Rais Obama kuhusu uhamiaji, yanatoa fursa kwa mamilioni ya wahamiaji wanaoishi nchini Marekani kinyume cha sheria kutorejeshwa makwao.
Majimbo ishirini na sita ya Marekani yameomba kusitishwa kwa sheria ya rais huku hatua zaidi za kisheria kuufutilia mbali mpango huo wa rais zikiendelea.
Bunduki waliyoporwa Polisi yapatikana Mapango ya Amboni Tanga
Bunduki waliyoporwa Polisi yapatikana Mapango ya Amboni Tanga
Jeshi la Polisi jijini Tanga limefanikiwa kuipata bunduki aina ya SMG, ikiwa na risasi 20 ndani ya mapango ya Majimoto katika eneo la Amboni.
Hatua hiyo inafauatia msako maalumu uliodumu kwa siku nne sasa, uliolenga kusaka silaha na wahalifu wanaodaiwa kujificha ndani ya mapango ya mawe yaliyopo Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akizungumza na waandishi wa Habari jijini Tanga jana amesema “Kutokana na taarifa kutoka kwa wananchi Februari 16 mwaka huu katika kitongoji cha la ‘Kona Z’ kilichopo Amboni, tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja ambaye kwa sasa sitamtaja jina kwa sababu upelelezi unaendelea, tulimhoji kwa kina akatupa taarifa kuhusu silaha hii,”
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa akiwemo aliyesababisha kupatikana kwa bunduki hiyo. Baadhi ya watu wanaendelea kuhojiwa, kupata taarifa kwa lengo la kukamata waliopora silaha kwa askari na kurushiana risasi kwenye mapango hayo.
Hata hivyo alikanusha taarifa zilizoenea mjini kwamba ipo miili ya wahalifu,iliyokutwa ndani ya mapango hayo, kutokana na mapigano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
HOUSES FOR SALE
HOUSE FOR SALE: Located at Bunju B with 2 bed rooms,sitting room and kitchen. It hase a servant quarter, fence and it has 360sqm. PRICE is TSH. 100 mil negotiable.
HOUSE FRO SALE: Located at Ununio, 7 bed rooms, 2 sitting rooms, kitchen, store at nd a libraly. It has a car parking it has a dept to I&M Bank. PRICE is TSH.250 mil negotiable.
HOUSE FOR SALE: A new house located at Kiluvya kwa Komba it has 3 bed rooms, sitting room, dinning room, kitchen and store. It has a servant quarter and outside kitchen, it has a fence with a shop frame. It has 1200 sqm, water supply from Dawasa, PRICE is TSH. 120 mil negotiable.
Tuesday, 17 February 2015
Chelsea, Bayern Munich zaambulia sare Ugenini
Chelsea, Bayern Munich zaambulia sare Ugenini
Magoli ya vipindi tofauti ya Branislav Ivanovic (36′) kwa upande wa Chelsea na Edinson Cavani (54′) yanazifanya timu hizo kugawana pointi huku Chelsea wakiwa na faida ya pointi ya ugenini na hivyo kusubiri mechi ya marudiano itakayofanyika darajani Stanford Bridge.
Mechi nyngine ya hatua ya mtoano imefanyika huko Ukraine kwenye uwanja wa Shakhtar Donetsk kwa Bayern Munich kutoka sare 0-0 na wenyeji Shakhtar Donetsk huku tukio kubwa likiwa kwa kiungo mkabaji Xabi Alonso kupewa kadi nyekundu ikiwa ni mechi yake ya 100 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Misri yaomba msaada UN kukabiliana na Islamic State
Misri yaomba msaada UN kukabiliana na Islamic State
Rais wa misri Abdel Fatah Al-Sisi ameutaka umoja wa mataifa kuidhinisha hatua za kijeshi za kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State pamoja na Jihadi nchini Libya.
Akizungumza na kituo kimoja cha radio cha Ufaransa ( Europe One) rais Sisi alisema kuwa watu nchini Libya wanataka hatua kali kuchukuliwa ili kuleta usalama na udhabiti nchini mwao. ”Hatutawaruhusu watoto wetu wachinjwe ovyo na hawa magaidi.” Al sisi alisema
Wito wa rais Sisi unakuja siku moja baada ya ndege za kivita za Misri kushambulia ngome za Islamic State kulipiza kisasi kuuawa kwa wamisri wa dhehebu la Coptic nchini Libya siku ya Jumamosi.
Hapo jana , Taarifa kutoka Misri zilisema kuwa, ndege za kijeshi ziliwashambulia wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakichinjwa.
Obasanjo atimuliwa PDP, achana kadi yake hadharani kwa hasira
Obasanjo atimuliwa PDP, achana kadi yake hadharani kwa hasira
Mgogoro umeibuka ndani ya chama tawala cha PDP kufuatia Rais wa
Zamani Bw. Olusegun Obasanjo kutimuliwa ndani ya chama kwa madai ya
kupinga vikali kuahirishwa kwa uchaguzi nchini Nigeria hadi mwezi machi.
Muda mchache kabla ya kutimuliwa chamani, Obasanjo aliwaambia waandishi wa Habari kuwa alikuwa akitarajia kutimuliwa chamani japo ujumbe ulimfikia mapema kabla ya tangazo.
Kwa hasira alichana chana kadi yake ya uanachama hadharani jambo lililowaaudhi makada wa rais kwani ilikuwa inaonesha mgawanyiko katika chama huku uchaguzi mkuu ukisogea.
Inadaiwa kuwa Rais wa sasa Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kukipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC) na mpinzani wake mkuu Buhari.
Rais huyo wa zamani amekuwa mstari wa mbele kumkosoa rais wa sasa Goodluck Jonathan, ambaye anawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha PDP.
Kwa upande mwingine, Jeshi la Nigeria limemlaani Olusegun Obasanjo na kusema kuwa ameliabisha jeshi kwa kuashiria kuwa walikuwa na njama ya kuongeza muda.
Muda mchache kabla ya kutimuliwa chamani, Obasanjo aliwaambia waandishi wa Habari kuwa alikuwa akitarajia kutimuliwa chamani japo ujumbe ulimfikia mapema kabla ya tangazo.
Kwa hasira alichana chana kadi yake ya uanachama hadharani jambo lililowaaudhi makada wa rais kwani ilikuwa inaonesha mgawanyiko katika chama huku uchaguzi mkuu ukisogea.
Inadaiwa kuwa Rais wa sasa Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kukipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC) na mpinzani wake mkuu Buhari.
Rais huyo wa zamani amekuwa mstari wa mbele kumkosoa rais wa sasa Goodluck Jonathan, ambaye anawania muhula wa pili kwa tiketi ya chama cha PDP.
Kwa upande mwingine, Jeshi la Nigeria limemlaani Olusegun Obasanjo na kusema kuwa ameliabisha jeshi kwa kuashiria kuwa walikuwa na njama ya kuongeza muda.
Mtoto mwingine mwenye ualbino atekwa nyara Geita
Mtoto mwingine mwenye ualbino atekwa nyara Geita
Maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino nchini Tanzania yanaendelea kuwa mashakani kufuatia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino kutekwa katika wilaya ya Chato mkoa wa Geita.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani humo limesema kuwa mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Yohana Bahati mwenye umri wa mwaka mmoja alitekwa nyumbani kwao na watu wasiojulikana jana usiku.
Habari zinasema watu waliokuwa na silaha za jadi waliwaweka chini ya ulinzi Bahati Misalaba na mkewe ambao ni wazazi wa mtoto albino ambaye walimteka na kutoweka naye.
Familia hiyo pia ina watoto wengine wawili wenye ulemavu wa ngozi, Tabu Bahati mwenye umri wa miaka miwili na Shida Bahati mwenye miaka kumi na mmoja ambao walinusurika kuchukuliwa na watu hao kwa sababu wakati unyama huo ukitendeka nyumbani kwao hawakuwepo walikwenda kucheza kwa majirani zao.
Inadaiwa kuwa Mama wa mtoto huyo alijeruhiwa vibaya wakati akimpigania mtoto wake asichukuliwe na watu hao.
Matukio ya ukatili dhidi ya alino yamesambaa katika mikoa yak kanda ya ziwa huku imani za kishirikina ikidaiwa ndiyo sababu kubwa inayaosababisha utekaji na mauaji kwa watu wenye ualbino.
Kufuatia tukio hilo Jeshi polisi limeanza msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kufanya kitendo hicho.
Subscribe to:
Posts (Atom)