Tuesday 21 July 2015

Hofu yatanda Uchaguzi wa Rais Burundi

Hofu yatanda Uchaguzi wa Rais Burundi

Tarehe July 21, 2015
Vurugu nchini Burundi.
Hofu imetanda nchini Burundi kufuatia kutokea ufyatulianaji wa risasi na milipuko usiku kucha nchini Burundi, usiku wa kuamkia uchaguzi wa rais uliozua utata.
Vurugu  hizo zinafuatia wananci kupinga  Rais Nkurunziza kuwania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi. Maeneo mengine risasi hizo zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo. Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Kwa mujibu wa mshauri wa kisasa wa rais, amesema haya ni mashambulio yanayofanywa na ‘magaidi’ wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuzwa.

clouds stream