Thursday 17 August 2017

SERIKALI YATOA TAARIFA YA AWALI KUUNGUA SOKO LA SIDO MBEYA


20881879_1580321795365142_350396105363380250_n
IMG-20170426-WA0006

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ametoa pole kwa wafanyabiashara wote walioathirika na janga la moto baada ya soko la Sido kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa Mhe. Makalla soko la Sido lilianza kuungua saa 21:32 jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko hilo.

Pamoja na kutoa pole amewashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano kwa kazi kubwa ya kudhibiti moto huo usiendelee na kuleta madhara makubwa zaidi.

“Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya imeunda kamati ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha moto huo. Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana,” amesema Mhe. Makalla.

Aidha, amesema kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu au kikudi cha watu.

“Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu,” amesisitiza Mhe Makalla.

clouds stream