Friday 4 August 2017

Raia wanapiga kura kuchagua kiongozi mkuu wa Rwanda

Uchaguzi Rwanda

IMG-20170426-WA0006

Raia nchini Rwanda wanamchagua kiongozi mkuu wa Rwanda katika uchaguzi mkuu Ijumaa, ambao unatarajiwa na wengi kumuongezea muhula mwingine madarakani rais Paul Kagame.

Frank Habineza wa chama cha Green Party na Philippe Mpayimana, ambaye ni mgombea huru pia wanawania urais katika uchaguzi huu.

Lakini wapinzani hao wote hawatarajiwi kumpa ushindani mkubwa Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2000.

Kuna hisia tofuati kuhusu utawala wake Kagame nje ya nchi hiyo.

Lakini uungwaji mkono mkubwa anaopata ndani ya Rwanda, unamhakikishia ushindi mkubwa katika uchaguzi huu.

Ameutaja uchaguzi huo kama mpangilio usio budi kufanyika.

Anasifiwa kwa kukuza uchumi wa taifa hilo.

Lakini wakosoaji wanamshutumu kwa kukandamiza upinzani na kuzuiwa uhuru wa kisiasa nchini.

Wagombea wengine wanasema wafuasi wao wamenyanyaswa lakini chama tawala kina kana tuhuma hizo.

Katiba ya Rwanda ilikarabatiwa mnamo mwaka 2015, na kumpa rais Kagame nafasi ya kushinda muhula mwingine wa miaka 7 na mihula mingine miwili ya ziada ya miaka mitano kila mmoja.

Kwa hivyo, ana nafasi ya kusalia madarakani hadi mwaka 2024.

clouds stream