Tuesday 29 August 2017

Msukuma Amvaa Tundu Lissu Sakata La Wanasheria Kugoma

msukum
IMG-20170426-WA0006

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma amejitokeza na kupinga wito wa mgomo ulioitishwa na Rais wa TLS na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Lissu siku ya Jumapili alitoa wito kwa Mawakili wote ambao ni Wanachama wa chama hicho kususia shughuli za Mahakama ili kushinikiza Jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika na tukio la kulipuliwa ofisi za IMMMA Advocates zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.

Msukuma amesema kitendo cha Chama cha Mawakili kutangaza mgomo ni kutowatendea haki wateja wao kwa siku zote watakazoamua kususia shughuli za Mahakama.

”Watanzania kwa pamoja tunalaani kitendo kilichofanywa kwenye Ofisi za IMMMA Advocates kwa sababu ni kitendo cha kinyama na kihalifu.Tunamuomba IGP Sirro afanye juu chini kuhakikisha watu hawa wanakamatwa.”Alisema Msukuma.

“Nilishtushwa sana na matamko yaliyotolewa na Rais wa TLS, Tundu Lissu kwamba anatangaza mgomo wa Wanasheria kuanzia kesho na keshokutwa. Najiuliza kama Tundu Lissu anatangaza mgomo wa Wanasheria, hiyo ndiyo hukumu ya kumpata mvamizi? Alihoji Msukuma.

clouds stream