Friday 18 August 2017

Mkapa Kushuhudia Kagame Akila Kiapo Leo

Rais. Paul Kagame wa Rwanda.
Rais. Paul Kagame wa Rwanda.
IMG-20170426-WA0006

Rais Mteule wa Rwanda, Paul Kagame anatarajiwa kula kiapo cha Urais leo baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika Agosti 4, mwaka huu kwa asilimia 98.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika watakaohudhuria sherehe hizo za kula kiapo ni Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye yupo nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo kusuluhisha mzozo wa kisiasa.

Sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Taifa wa Amahoro, zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali.

Kagame atakuwa anaanza muhula wa kwanza wa miaka saba tangu taifa hilo lilipofanyia marekebisho katiba yake.

Viongozi wengine watakaohudhuria sherehe hizo ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Rais wa Niger, Mahaadou Issoufou, Rais wa Senegal, Macky Sally, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Congo Brazaville, Sassou Ngueso

clouds stream