Wednesday 2 April 2014

HTC ONE (M8) YAANZA KUONGELEWA. ITS EVEN BETTER THAN THE ORIGINAL.

Tokea HTC watoe simu yao ya HTC one na kuitangaza kwa nguvu zote katika masoko mengi, HTC wamepata faida kubwa sana na pia wameweza kuteka soko la nchi kama Thailand kwa mauzo ya smart phones.
Sasa kama uliipenda HTC One basi utaipenda zaidi HTC One (M8). Hii ni sababu ya kua HTC (M8) inatarajiwa kua na kasi zaidi na uwezo mkubwa zaidi kuliko ile ya awali. Haya ndio mambo ya kutarajia katika M8.

1. MUUNDO


HTC wanasema kua M8 ni simu ambayo kwa asilimia 90 imeundwa kwa chuma (metallic). Pia imeundwa kwa kutumia alluminium abapo itahakikisha kua mtu anapata kitu imara iwapo atakinunua. Kwa M8, HTC wameweka speaker zenye sauti zaidi kiasi kwamba kama ni mpenzi wa kutizama movie kwa njia ya simu, basi burudani inakua iko mkononi mwako.

2. SCREEN.

HTC wameongeza ukubwa wa screen kutoka inchi 4.7 mpaka 5 kwa simu hii ya M8. Ukubwa huu unamaanisha vitu viwili, kwanza unapata nafasi zaidi katika screen yako na pia muonekano wa picha na video unakua mzuri zaidi.

3. UTENDAJI KAZI

M8 Imetengenezwa kwa jinsi ya kua itakaa na charge zaidi, itaweza kuhifadhi vitu vingi zaidi na pia itakua na uwezo mkubwa sana wa internet.

4. KAMERA MBILI KWA NYUMA.

Unaweza kujiuliza kwanini niwe na kamera mbili kwa nyuma ila M8 imeweka kamera mbili ili kumsaidia mpiga picha kuweza kupata uhakika wa picha zake kwa upana na urefu pia. Pamoja na kamera za M8 kua mbili zina uwezo mkubwa sana.

5. SPECIFICATIONS

Key Features:

  • 5in Full HD Screen
  • Snapdragon 801 Chip
  • 2GB RAM; 16GB Storage
  • MicroSD Card
  • Android 4.4 w/ Sense 6.0
  • Price as Reviewed: £530

clouds stream