Tuesday 22 April 2014

Wanafunzi 230 bado wametekwa Nigeria


Takriban wanafunzi 230 wa shule iliyoshambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram, hawajulikani waliko.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya maafisa wakuu wa shule ya Chibok katika jimbo la Borno wanaosema kuwa wanafunzi hao hawajapatikana tangu wavamizi walipovamia shule yao wiki jana.
Maafisa wakuu wa shule katika jimbo la Borno wanasema kuwa takriban wanafunzi 230, hawajulikani waliko.Idadi hii iliyotolewa na maafisa wa shule inakinzana na idadi iliyotangazwa na serikali hapo awali ya wasichana 85 kutopatikana.
Walitekwa nyara katika eneo la Chibok, wiki jana na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Idadi hii ni kubwa ikilinganishwa na idadi iliyotangazwa na serikali.
Mwalimu mkuu wa shule ambako wanafunzi hao walikuwa wanasoma, ameambia idhaa ya Hausa ya BBC kuwa sajili la wanafunzi katika shule hiyo, linaonyesha kuwa wanafunzi wengi bado hawajapatikana.
Anasema, idadi ya wasichana ambao hawajapatikana, imetokana na idadi ya wazazi waliosajiliwa wakisema kuwa watoto wao ni miongoni mwa wale walioyekwa nyara.
Ni wanafunzi 43 pakee wameweza kupatikana baada ya kutoroka kutoka mikononi mwa washukiwa wa Boko Haram.
Idadi hiyo kubwa imejitokeza wiki moja baada ya utekaji nyara wa wanafunzi katika jimbo la Borno na pia baada ya gavana wa jimbo hilo alisisitiza apelekwe huko chini ya ulinzi wa jeshi.
Wazazi walimwambia kuwa maafisa wa ulinzi hawakutaka kuwasikilizawalipotaka kuwasilisha orodha ya majina ya watoto wao ambao idadi yao ilifika 234.
Sababu ya tofauti katika takwimu hizo bado haijabainika
Takriban watu 1,500 wameuawa na Boko Haram mwaka huu. Wapiganaji hao wanapigania kile wanachosema ni elimu ya kimagharibi na wanataka sheria za kiisilamu kutumia kuitawala nchi hiyo.

clouds stream