Friday 11 April 2014

MANENO YENYE UTATA YA JOSE MOURINHO AKIWA CHELSEA.


1. Wachezaji wadogo ni kama matikiti madogo, mpaka uyakate na kuyaonja ndio utakua na uhakika ya kwamba ni mazuri. Kuna muda tikiti linaweza kuonekana zuri ila ukilila unajua kua ni baya na mengine yenye muonekano mbaya ndio matamu zaidi. Ni kitu kimoja kuongelea wachezaji wadogo na kingine kuongelea mpira ya kulipwa. Daraja leo kuvuka ni gumu sana, inabidi wajifunze na kufanya mazoezi sana.

2. Makelele sio mchezaji mpira- makelele ni mtumwa. Amewai kucheza mpira katika kiwango kikubwa sana ikiwemo  fainali ya mechi ya kombe la dunia na sasa anataka kustaafu kuchezea Ufaransa na kocha anasema kua asipochezea Ufaransa hatochezea Chelsea. Tunazijua sheria. Wewe sio mtumwa, una haki zako. Alisema haya aliwauponda uongozi wa soka la kulipwa Ufaransa.

3. Akiongelea kuhusu Andre Shevshenko kutofunga aliwaambia waandishi wa habari kua " ili kuwanyamazisha nawaambia hivi, akiendelea kutokufunga bado ataendelea kucheza.

4. Ricardo Carclyo anamatatizo ya akili, ningeshauri afanyiwe uchunguzi au apelekwe hospitali akatibiwa. Alisema hivi baada ya Ricardo kulalamika kutokupangwa.

clouds stream