Monday 18 January 2016

Mhariri Mkuu Afunguka Kufutwa Gazeti La Mawio


Mhariri Mkuu Afunguka Kufutwa Gazeti La Mawio


Tarehe January 18, 2016
.
1 (2)

Mhariri Mkuu wa gazeti la Mawio  ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Victoria Media inayolimiliki gazeti hilo Bw. Simon Mkina ameeleza jinsi walivyopokea taarifa ya kufungiwa gazeti lake Maisha.
Adha, Jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye alitangaza  kuwa gazeti hilo limefutwa kutokana na kuandika habari za uchochezi na zenye utata na kwamba wamiliki wa gazeti hilo wamekuwa wakionywa na serikali tangu mwaka 2013 lakini hata majibu yao yalikuwa ya kiburi na dharau.
Akizungumzia hatua hiyo  Mkina amesema kuwa ingawa wamekuwa wakisikia habari za kufutwa kwa gazeti lao kweye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, bado hawajapata taarifa rasmi kutoka serikalini kuhusu uamuzi huo ili wajue hatua watakazoweza kuchukua.
Amesema kuwa uongozi wa kampuni hiyo umepanga kukaa na kufikiria hatua sahihi za kuchukua kutokana na uamuzi huo na kuitaka serikali kuwapa taarifa ya maandishi kuhusu sababu zilizopelekea kufutwa kwa gazeti lao na habari iliyosababisha wafutwe.
Ameongeza kuwa Kampuni yake  inashindwa kufahamu ni habari gani ilisababisha wafutwe kwa kuwa walikuwa wakipokea barua ya kujieleza karibia kila baada ya wiki mbili kuhusu habari walizokuwa wanaziandika.

clouds stream