Monday 18 January 2016

Sahara Media Group Yaijibu TCRA, Kufungiwa Star Tv

Sahara Media Group Yaijibu TCRA, Kufungiwa Star Tv

Tarehe January 17, 2016
Anthony Diallo mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group.
Anthony Diallo mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group.
Kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki   Star Tv, RFA  na Kiss Fm  imebuka na kuishangaa  mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA  iliyoitaka  kampuni hiyo kufunga vyombo vyake vyote vya habari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TCRA imevitaja vyombo vya habari 21 ikiwemo Star TV, Redio Free Afrika na Kiss FM kwa madai ya kutolipia ada ya leseni.
Wakizungumzia  kufungiwa na TCRA Manejimenti ya sahara media group  imesema kuwa haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka TCRA  ya kutakiwa kufunga vyombo vyake.
Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 hadi kufikia mwezi October 2015.
Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.
Hata hivyo  menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa  vyombo vya habari bila kujali athari za kufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.
Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.
Menejimenti pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki na kuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.
Menejimenti ya star tv  imewaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake  kufuatia  kuanza kulishughulikia suala hilo kati yake na TCRA.

clouds stream