Friday 22 April 2016

Asilimia 79 Ya Simu Zinazotumiwa Na Watanzania Ni Halali


Asilimia 79 Ya Simu Zinazotumiwa Na Watanzania Ni Halali


Tarehe April 22, 2016
1
meneja uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa kipindi cha desemba hadi February mwaka huu ni halali, huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia.
Akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya  namba za utambulisho wa simu za kiganjani, meneja uhusiano wa TCRA, Innocent Mungi amesema kutokana na elimu ambayo wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu  hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo ya aina yeyote.
“Wakati tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30 zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu bandia zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache mno,” aliongeza.
Aidha, Mungi alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu  na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.
Awali mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Ally Simba aliwataka wananchi kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa watumiaji wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia.

clouds stream