Wednesday 6 April 2016

Madrid Chalii Yapigwa 2-0 Na Wolfsburg

Madrid Chalii Yapigwa 2-0 Na Wolfsburg

Tarehe April 7, 2016
Ronaldo akiwa hoi baada ya timu yake kung'olewa kwenye michuano ya vilabu bingwa Ulaya
Ronaldo akiwa hoi baada ya timu yake kung’olewa kwenye michuano ya vilabu bingwa Ulaya
REAL Madrid imepoteza mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa mabao 2-0 usiku wa Jumatano na wenyeji VfL Wolfsburg Uwanja wa Volkswagen Arena.
Ikitoka kushinda 2-1 dhidi ya mahasimu Barcelona katika La Liga, Real inayofundishwa na Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa, Zinadine Zidane ilishindwa kufurukuta Ujerumani.
Mabao ya Wolfsburg yamefungwa na Ricardo Rodriguez kwa penalti dakika ya 18 na Maximilian Arnold dakika ya 25 na sasa Real wanatakiwa kushinda 3-0 nyumbani wiki ijayo ili kwenda Nusu Fainali.

clouds stream